Mwanamuzi wa Rwanda Meddy afungwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa

Mwanamuziki maarufu wa Rwanda Meddy ametiwa nguvuni baada ya kukamatwa akendesha gari huku akiwa ni mlevi , imesema polisi mjini Kigali.
" Alikamatwa alipokuwa akiendesha gari kwa kasi kupita kiasi huku akiwa amelewa, atafungwa kwa siku tano na kupigwa faini ya ya Franga za Rwanda 150,000 sawa na $150," msemaji wa polisi mjini Kigali Goretti Umutesi, ameiambia BBC.
Meddy ambaye jina lake halisi ni Ngabo Medard ni msanii wa muziki wa R&B, mnyarwanda anayeishi nchini Marekani aliiambia BBC mwezi Agosti kwamba alikuwa anapanga kufanya tamasha nchini Rwanda na mataifa mengine ya Afrika.
Katika miezi ya hivi karibuni polisi ya Rwanda imeimarisha msako dhidi ya watu wanaoendesha magari wakiwa wamekunywa pombe ili kukabiliana na ajali za barabarani.
Wiki mbili za mwezi Septemba watu 191 walikamatwa na kupigwa faini kwa kunywa pombe na kuendesha magari, na mwezi Agosti zaidi ya watu 700 walishtakiwa kwa kosa hilo.
Licha ya kulipa faini ya dola $150, baadhi ya washukiwa wamekuwa wakifungwa kwa siku kadhaa, hatua ambayo imekuwa ikikosolewa kuwa ni kinyume cha sheria.
Wakosoaji pia wanasema badhi ya polisi hawana kipimo cha kupima kiwango cha pombe alichokunywa mtu na kuthibitisha kwamba madereva wamekiuka viwango vya pombe kinachopaswa kuwa katika damu.
Unaweza kusoma pia:
Licha ya ukosoaji huo, Bi Mutesi ameiambia BBC kuwa msako huo wa madereva wanaoendesha magari huku wakiwa wamekunywa pombe utaendelea ili kuhakikisha barabara ziko salama.
Wimbo wake maarufu Slowly una zaidi ya watazamaji milioni 18 katika YouTube.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa YouTube ujumbe
Kwa mujibu wa polisi kiwango cha 0'08 cha kileo katika damu ndicho kinachokubalika kwa mtu anayeendesha gari nchini Rwanda. Kiwango cha kileo mwilini hupimwa na kifaa kinachofahamika BAC na hupima kulingana na uzito wa mtu aliyekunywa pombe.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Katika baa nyingi yamewekwa matangazo yanayowakumbusha watu wasiendeshe magari wakati wamekunywa pombe.
Wamiliki wa baa nao wameagizwa kuwakumbusha na kuwaonya wateja wao pale wanapowaona wanabugia pombe kwa kiwango cha juu.















