Mwanamke anayetaka kila mtu afurahie ngono...Sio wanaume pekee

Chanzo cha picha, Erika Lust Productions
"Wanawake pia wana hisia wakati wanaposhiriki tendo la ndoa."
"Sote tuliopo duniani tumetokana na tendo la ndoa," anasema Erika Lust, muelekezi mkuu wa filamu za ngono anayemiliki kampuni ya kutayarisha filamu.
Wanawake wanataka kufurahia filamu za ngono sawa na wanaume, lakini "filamu nyingi za ngono zimetayarishwa na wanaume ambao hawajali hisia za wanawake,"anasema.
"Filamu zangu, zinajaribu kupeana mbinu mbadala tofauti na filamu za ngono zilizozoeleka."
Kila sekunde, zaidi ya watu 1,000 wanatembelea mitandao ya inayoonesha filamu za ngono (kwa mujibu wa data ya mwaka 2018 ya mtando wa PornHub).
Lakini filamu nyingi zinazopatikana kwa urahisi mitandaoni zinaangazia vitendo vya ngono vinavyolenga kumfurahisha mwanamume bila kujali hisia ya mwanamke anayeshiriki tendo hilo'' anasema mtayarishaji filamu huyo.

Erika Lust anaongeza kuwa mtu anahitaji kutembelea mitandao hiyo kujionea ujumbe katika maudhui ya filamu za ngono zinazonadiwa hapo: "'Mlatino mnene anavyoshughulikiwa', yaani wanatumia maneno ya kumdhalilisha mwanamke... hiyo ni nini! Kama maneno hayo yanalenga kumvutia mtu, hapo wamekosea."
"Ngono inatakiwa kuwa kitendo kinachowaleta pamoja watu wawili, walioamua kufurahia muda wao pamoja."
Lisa Williams, mmoja wa waandaaji wa kipindi cha ''The Hot Bed'' mtandaoni na mwandishi wa kitabu cha masuala ya ngono kinachofahamika kama ''More Orgasms'' anakubaliana na wazo hilo .
"Wasikilizaji na wasomaji wetu wanasema kuwa wanakumbana na filamu za ngono mitandaoni ambazo wanahisi haiangazii hisia zao," anasema, "Haziwakilishi furaha ya mwanamke, kile anachotaka na jinsi angelipenda kuhudumiwa."
Instagram na ripoti za 'kufuta ujumbe'

Chanzo cha picha, Instagram / @cecile_hoodie
Japo Erika anatumia mitandao ya kijamii kutangaza filamu zake za ngono, anasema kuwa anakabiliwa na changamoto nyingi - kwasababu ya watu wanaofanya kazi kama yake - ''unahitaji kujitolea sana''
Erika anasema mitandao ya kijamii hupiga marufuku baadhi ya picha anazotumia kunadi kazi yake na ya wenzake wanaotumia ubunifu wa hali ya juu kuwasilisha ujumbe wa ngono.
Erika anaamni kuwa akaunti yake na ujumbe anaotuma katika mtando wa Instagram "umefungiwa" - kumaanisha ujumbe wako umepigwa marufuku au kudhibitiwa kwa kiwango fulani - kwa kuwa na ''maudhui ya ngono".
Alipolalamikia hatua hiyo mtandaoni, watayarishaji wengine wa filamu za ngono waliunga mkono madai hayo.
Instagram iliiambia BBC hawatumii mfumo huo kudhibiti ''maudhui'' lakini "inachukua hatua dhidi maudhui inayolalamikiwa" ikiwa ikikiuka maadili - pia inasema watumiaji walioathiriwa na hatua hiyo wana fursa ya kukata rufaa dhidi ya hatua iliyochukuliwa na mtandao huo.
Lakini Lisa anasema akaunti yake @thehotbedcollective katika mtandao wa Instagram - ambayo inajitambulisha kama ukumbi wa kutoa elimu kuhusu masuala ya ngono - pia imeathirika na marufuku hiyo.
"Ujumbe wetu ulifutwa baada ya watumiaji wa mtandao huo kulalamikia maudhui yake, japo hatua hiyo haikuwa na msingi wowote. Tuliweka mchoro wa mwanamke anayejichua, ambao ulifutwa mara moja."
"Inaonekana kuna upendeleo," anasema Lisa, "ujumbe huo ulikuwa maudhui yanayolenga wanawake ili iwasaidie kuelewa miili yao".

Chanzo cha picha, Getty Images
Zaidi ya thelutjhi moja ya wanawake wanasema wamejifunza kuhusu ngono kupitia filamu za ngono kwa mujibu wa Kulingana na data za ( utafiti wa BBC mwaka 2019, nchini Uingereza), huku 53% ya wavulana wakiamini kuwa filamu za ngono mitandaoni ni za kweli (Utafiti wa NSPCC mwaka 2017, data ya Uingereza).
"Kuna pengo kubwa la ukosefu wa ufahamu kuhusu masuala ya ngono katika jamii, hali inayofanya vijana wadogo kugeukia filamu za ngono,"anasema Erika.
"Wana hamu ya kujua mengi kuhusu ngono, wanataka kuelewa mabo yote yanazunguka tendo lenyewe... ndio sababu wanatazama filamu za ngono."













