Wanunuzi wa bidhaa za ngono wanaongezeka sana

maduka ya ngono
Maelezo ya picha, si rahisi kuonana na majirani katika maduka hayo

Maelfu ya watu huendesha magari hadi katika eneo la A1 kila siku, huenda kununua vitu mbalimba kama vyakula na kujaza mafuta ya gari katika eneo hilo lenye pilika pilika nyingi, lakini hufuata nini hasa? na nani anaenda?

nguo za ndani, kamba za kufunga, vifaa vya ngono na midoli ya kufanyia ngono, vyote hivi huuzwa karibu na kituo cha kujazia mafuta katka mitaa ya northbound.

kuna maduka zaidi ya saba ya bidhaa hizo za watu wazima, hii ilimfanya mchekeshaji mmoja kuandika katika ukurasa wa Twitter '' hivi madereva eneo A1 huwa wana ashiki kiasi gani?''

lakini kwanini barabara ndefu zaidi ya uingereza imegubikwa na maduka ya bidhaa za ngono?

''maduka ni mazuri kwa namna mbalimbal'' amesema Graham Kidd mmoja wa wamiliki wa duka kwa miaka 11 sasa , ''kuna sehemu nzuri ya kuegesha magari, na ni sehemu zenye usiri sio rahisi kukutana na jirani yako.

''tusisahau kuwa kuna uoga wa namna fulani mtu kukutwa katika maduka ya bidhaa za ngono, hivyo yakiwa mbali kama hivi unapata ujarisi wa kuja''.

duka

Chanzo cha picha, Google

Maelezo ya picha, moja ya duka likiwa mbali na makazi ya watu

Maduka haya yapo mbali na eneo la makazi ya watu, mbali na shule pamoja na mji, hivyo si rahisi kwa watu kuyalalamikia. ndani ya maduka kumepangwa vizuri na ya kisasa. yapo mbali na maduka mengine ya kawaida.

''tulipofungua duka kwa mara ya kwanza pembezoni mwa barabara, hatukujua kama itakua na mafanikio alisema bwana Kidd ''watu walikosoa kwa mara ya kwanza kwa sababu hawakujua wachukulie vipi , na sio kama tupo karibu na shule hapana''.

Michaela Snell
Maelezo ya picha, Michaela Snell anasema kuwa duka la Grantham linavutia watu wa aina mbalimbali

Maduka ya bidhaa za ngono, yanalenga sana wanaume zaidi kuliko wanawake, wao hununua vifaa vya ngono katika sherehe ambazo wanaume wanakua hawaalikwi. ''tulidhani kuwa kuna umuhimu sasa wa kufungua duka hili ili wenza waje kununua pamoja vifaa vya kujifurahisha wakati wa tendo la ndoa'' aliongeza bwana Kidd.

Zaidi ya watu 500 hutembelea kila wiki katika maduka hayo, Michaela Snell amesema kuwa asilimia 25% wanaofika dukani hununua bidhaa za aina mbalimbali , wengine huja tu kuembelea.

Merchandise
Maelezo ya picha, baadhi ya wanunuzi hupenda kuingia dukani ili kuchagua bidhaa mbalimbali

baadhi ya wateja wao huenda sehemu ambazo hazina bidhaa nyingi za kutisha wakati wengine wakienda moja kwa moja katika sehemu ya vifaa vya ngono.

''huwa tunawasalimia, wengine wanaitikia vizuri lakini wengine wanaogopa na kuenda moja kwa moja kwenye manunuzi, tunapata watu wa aina tofauti hapa'' anasema bi Snell.

kwa mujibu wa tafiti iliyofanyika na kampuni ya kinga (kondom), asilimia 79 ya wanawake na asilimia 58 ya wanaume walioshiriki wanasema kuwa wamewahi kutumia vifaa vya kingono (sex toys).

Sio lazima kwa wanunuaji kwenda katika maduka, kuna njia za mtandao pia ambazo hutumika kununua bidhaa.

Wanunuzi walionda na wapenzi wao wanasema walikubwa na uoga mkubwa kwa mara ya kwanza.

Merchandise
Maelezo ya picha, sehemu ya nguo ndio kimbilio kwa wanunuzi wengi wenye uoga

Richard Longhurst, mwanzilishi mwenza wa duka la Loveyhoney anasema kuwa mchanganyiko wa bidhaa unawapa nafasi ya kuchagua wanunuzi.

Bwana Kidd anasema kuwa duka lao linapata watu wengi wanokuja kuliko wanaonunua kupitia mtandaoni.

Real life doll
Maelezo ya picha, mdoli wa kufanyia ngono ndio bei ghali zaidi

katika miaka 12 bi Snell anasema kuwa amekua na kampuni hiyo, kufanya kazi kwenye maduka ya bidhaa za ngono kumemsaidia sana kujua masuala ya ngono.

''ninafurahi sana kufanya kazi hapa, nilifanya maamuzi sahihi, nafurahia sana.