Utafiti: Kutembea pole pole ukiwa na miaka 45 'ni dalili ya uzee'

Commuters walking quickly

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanaotembea pole pole 'huzeeka' ubongo na mwili, utafiti wagundua

Kasi ya kutembea ya watu waliofikisha umri wa miaka 40 ni ishara ya jinsi ubongo na miili yao, inavyozeeka, wanasayansi wanasema.

Kwa kutumia kasi ya kutembea, watafiti waliweza kupima hali ya mtu kuzeeka.

Watu wanaotembea pole pole 'huzeeka haraka - na nyuso zao pia huonesha kuzeeka sawa na bongo zao kuwa ndogo.

Watafiti hao pia wanasema matokeo ya uchunguzi huo "ulikua wa kushangaza".

Madaktari hutumia uwezo wa kutembea kubaini afya ya mtu kwa ujumla, hasa kwa watu walio na miaka zaidi ya-65, kwasababu ni chanzo kikuu cha kupima nguvu ya misuli, utenda kazi wa mapafu, uti wa mgongo na nguvu ya macho.

Kutembea pole pole ukiwa mzee pia kumehusishwa na na hatari ya kupoteza uwezo wa kukumbuka.

'dalili ya tatizo'

Katika utafiti huu, kati ya watu 1,000 nchini New Zealand - waliozaliwa katika miaka 1970na waliofuatiliwa hadi miaka 45 - mwendo wao ulibadilika mapema.

Kama muendelezo wa utafiti washiriki pia walifanyiwa vipimo vya mwili na jinsi bongo zao zinavyofanya kazi kadri miaka yao ilivyoendelea kuongezeka.

"Utafiti huu megundua kuwa kuwa kutembea pole pole ni tatizo ambalo limekuwepo kwa miongo kadhaa hata kabla ya kuzeeka," alisema Prof Terrie E Moffitt, mmoja wa watafiti hao kutoka chuo kikuu cha London na kile cha Duke nchini Marekani.

Watafiti walipima kasi ya kutembea ya walioshirika katika uchunguzi huo

Chanzo cha picha, Duke University

Maelezo ya picha, Watafiti walipima kasi ya kutembea ya walioshirika katika uchunguzi huo

Hata wale walio katika miaka yao ya 45, walionesha tofauti kubwa katika kasi yao ya kutembea huku yule alietembea haraka zaidi akitembea kwa mita mbili kwa sekunde (bila kukimbia).

Kwa jumla washiriki waliotembea pole pole walionesha dalili ya "kuzeeka haraka" huku mapafu, meno na kinga ya miili yao ikiwa chini ikilinganishwa na watu wanaotembea haraka.

Uhusiano wa hali hii na mtindo wa maisha

Kundi la kimataifa la watafiti wa kimataifa JAMA Network Open, limesema tofauti inayojitokenza katika uwezo wa ubongo kufanya kazi huenda unatokana na mtindo wa maisha ya mtu binafsi.

Lakini pia linadai kuwa dalili ya kuzeeka mapema inachangiwa na hali ya afya ya mtu alipokuwa mdogo.

Watafiti wanasema kupima kasi ya kutembea ya mtu akiwa mdogo ni njia itakayosaidia kutafuta tiba ya kudhibiti hali ya binadamu kuzeeka haraka.

Tiba kadhaa imetolewa ikiwa ni pamoja na kuzingatia liche lililo na kiwango cha chini cha mafuta na kutumia dawa ya inayofahamika kama metformin.

Tiba hiyo ipo katika hatua ya uchunguza.