Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 22.10.2019: Pochettino, Ferguson, Giroud, Eriksen, Abraham, Fred

Mauricio Pochettino

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kocha wa Tottenham,Mauricio Pochettino(katikati)

Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino, anasema kuwa anahofia kufutwa kazi kutokana na matokeo mabaya ya klabu hiyo (Mirror)

Juventus na Atletico Madrid zinamfuatilia beki wa West Brom wa miaka 19, Nathan Ferguson.(Sun)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33, anatakiwa na Crystal Palace na huenda akajiunga na klabu hiyo ifikapo mwezi Januari. (Daily Star)

Olivier Giroud

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Olivier Giroud

Real Madrid haitajaribu kumsaini mchezaji wa safu ya kati wa Tottenham raia wa Denmark, Christian Eriksen, 27, mwezi Januari hadi watakapowauza wachezaji wasiokuwa katika kikosi cha kwanza. (AS)

Real itaipatia Spurs kiungo wao wa kati wa Uhispania Isco, 27, na mshambuliaji wa Jamuhuri ya Dominica Mariano Diaz, 26, katika juhudi ya kupata saini ya Eriksen. (El Desmarque - in Spanish)

Mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham, 22, anakaribia kutia saini mkataba mpya wa kusalia Stamford Bridge baada ya kufunga mabao manane katika ligi ya Premia msimu huu. (Daily Star)

Isco

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Isco, Kiungo wa kati wa Real Madrid

Barcelona imemaliza mzozo wake na Atletico Madrid kuhusu usajili wa Antoine Griezmann, 28, kwa kumlipia euro milioni 15 zaidi mshambuliaji huyo wa Ufaransa. (El Mundo - in Spanish)

Derby itampatia nahodha wa zamani wa England Wayne Rooney, 33, mafunzo maalum kuhakikisha yuko tayari kwa mashindano atakapojiunga na klabu hiyo kutoka DC United. (Mail)

Kiungo wa kati wa Brazil na Manchester United Fred, 26 - ambaye alinunuliwa kwa kima cha £47m kutoka Shakhtar Donetsk mwezi Juni 2018 - anaamini kuwa ameanza kupata uzoefu wa soka la Uingereza. (Telegraph)

Antoine Griezmann

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Antoine Griezmann

Arsenal inaongoza katika kinyang'anyiro cha usajili wa beki wa RB Leipzig na Ufaransa wa chini ya miaka-21 Dayot Upamecano, 20, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa euro milioni 50. (Mail)

Meneja wa Italia Roberto Mancini huenda akamjumuisha kipa mkongwe wa Juventus Gianluigi Buffon, 41, na kiungo wa kati wa Boca Juniors wa miaka 36 Daniele de Rossi katika kikosi cha Euro 2020. (Rai Sport via Mail)

Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema anataka kusalia klabu hiyo maisha. (Marca)

Zinedine Zidane

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane

Beki wa zamani wa Arsenal na England Sol Campbell, 45, anafanya mazungumzo ya kuwa mkufunzi wa Southend, inayoshiriki soka la daraja ya kwanza - miezi miwili baada ya Macclesfield inayocheza soka ya daraja la pili. (Sun)

Tetesi Bora Jumatatu

Real Madrid inawafuatilia winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19 na mshambuliaji wa Norway wa miaka 19- Erling Braut Haaland, anayechezea Red Bull Salzburg. (El Desmarque, via Mail)

Jadon Sancho

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Jadon Sancho

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anataka kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na RB Leipzig Timo Werner,23 ambaye aliwahi kuhusishwa na tetesi za kujiunga na Liverpool. (Express)

Manchester United pia inajiandaa kumpatia mkataba mpya kiungo wa kati wa Uingereza Angel Gomes, 19, licha ya tetesi kuwa Barcelona inamtaka. (Sun)

Frank Lampard

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Meneja wa Chelsea Frank Lampard

Meneja wa Chelsea Frank Lampard anataka mshamsmbuliaji wa Ufaransa wa miaka 33, Olivier Giroud, ambaye hajafurahishwa na hatua ya kutojumuishwa katika kikosi cha kwanza aendelee kusalia Stamford Bridge. (Telegraph)

Chelsea imemuongeza mchezaji wa safu ya kati wa Atalanta na Ukraine Ruslan Malinovskyi, 26, katika orodha ya wachezaji amabao huenda wakahamia klabu hiyo msimu ujao wa joto. (Express)