Mfalme wa Thailand amvua vyeo mke wake kwa 'kutokuwa mwaminifu'

Mfalme wa Thailand Vajiralongkorn amemvua mkewe vyeo vyake kutokana na "tabia mbaya na kutokuwa mwaminifu kwa ufalme ".

Aliteuliwa mwezi Julai , miezi miwili tu baada ya mfalme kumuoa Queen Suthida, mke wake wa nne.

Tangazo rasmi lilisema kuwa Sineenat Wongvajirapakdi alikuwa "mwenye tamaa " na alijaribu "kujiweka katika hadhi ya malkia ".

"Tabia ya ya mke wa mfalme zilichukuliwa kama ukosefu wa heshima ," ilisema.

Unaweza pia kusoma:

Sineenat, ambaye alikuwa Meja Generali na rubani aliyesomea , muuguzi na mlinzi , alikuwa mtu wa kwanza kutunukiwa cheo cha Mke Mtukufu wa Ufalme.

Malkia Suthida - mwenye umri wa miaka 41- ambaye alikuwa mhudumu wa zamani wa ndege na naibu mkuu wa kikosi cha walinzi wa kifalme - ni mpenzi wa muda mrefu wa is King Vajiralongkorn's na amekuwa akionekana kuwa nae hadharani kwa miaka mingi.

Tangazo la kuvuliwa vyeo kwa Sineenat lilichapishwa katika jarida la Ufalme Jumatatu.

Kuanguka kwake kutoka cheo cha juu katika ufalme wa Thailand ni mabadilikoya ghafla ya hadhi yake ya juu aliyokuwa nayo ndani ya Ufalme. Kwa miaka mingi mara kwa mara amekuwa akionekana kando ya Mfalme Vajiralongkorn, na aliaminiwa kuwa ndiye mtu aliyekuwa karibu nae kuliko mtu mwingine.

Hata baada ya kmuoa malkia Suthida, Sineenart alikuwa ndiye mtu aliyeonekana zaidi na kuheshimika katika matukio ya kifalme.

Ufalme umesema nini ?

tangazo la ghafla la Jumatatu lilisema kuwa "alionyesha pingamizi na shinikizo kwa njia zote katika kuzuwia uteuzi wa Malkia "kabla ya harusi ya mwezi May.

"Mfalme alimpatia cheo cha mshauri wa ufalme, akiwa na matumaini ya kuondoa msukumo na matatizo ambayo yangeweza kuathiri ufalme ," lilisema tangazo.

Lakini liliongeza kuwa kuwa Sineenat alionyesha "upinzani dhidi ya mfalme na Malkia " na kukiuka mamlaka kwa kutoa amri kwa niaba ya kwa niaba ya mfalme.

Mfalme ,taarifa ilisema alibaini kuwa "hakuwa mwaminifu kwa mamlaka aliyopewa, na wala hakuwa na maadili yanayofaa kulingana na hadhi yake ."

Aliamuru aondolewe vyeo vyake vyote vya kifalme, hadhi yake katika kikosi cha walinzi wa Ufalme na vyeo vyake vya kijeshi.

Mfame Vajiralongkor alitrawazwa kuwa mfalme baada ya kifo cha baba yake mwaka 2016.

Ni vipi kuhusu wake wa Mfalme?

Alikuwa na wanawame wanee - Malkia Soamsawali kuanzia 1977 hadi 1993; Yuvadhida Polpraserth kuanzia mwaka 1994 hadi 1996; Srirasmi Suwadee kati ya mwaka 2001 na 2014; na Mfalme Suthida.

Sababu ya kweli ya kuanguka kwa Sineenart huenda isiwekwe wazi kwa umma, ikizingatiwa usiri unaotawala masuala ya kasri ya Ufalme wa Thailand.

Sheria ya Ufalme inayozuwia kuutukana ufalme, ni miongoni mwa sheria kali zaidi duniani.

Lakini kuvuliwa mamlaka kwa Sineenat kunafanana na yale yaliyowakuta wake wawili wa zamani wa mfalme huyo.

Mwaka1996, alimkataa mke wake wa pili ambaye ilibidi atorokee Marekani , ambako amekuwa akiishi tangu wakati huo na akawakataa watoto wake wanne aliozaa nae.

Mwaka 2014, mke wake watatu Srirasmi Suwadee pia alivuliwa vyeo vyake vyote. Mvulana wake wa miaka 14 amelelewa na mfalme Vajiralongkorn Ujerumani na Uswiss

Mfalme ametekeleza majukumu yake ya kifalme kwa mfumo wa moja kwa moya kuliko watangulizi wake wa hivi karibuni.

Mapema mwezi huu , vikosi viwili muhimu vya kijeshi katika mji mkuu Bangkok wviliwekwa chini ya usimamizi wake moja kwa moja na mamlaka ya kijeshi yamewekwa zaidi mikononi mwa Ufalme jambo ambalo halijawahi kutokea katika Thailand ya sasa.