Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kioja cha familia ya rais Buhari: Harusi bandia, rais na mgogoro wa kifamilia
Familia ya kwanza nchini Nigeria , ya rais Buhari ipo ndani ya hadithi inayofanana na vipindi vingi vya siku ya Jumapili kuhusu familia.
Ni hadithi kuhusu rais huyo kuchukua mke wa pili - ambaye anadaiwa kuwa waziri huku mkewe akitoa hasira zinzaodhihirisha ugomvi wa ndani
Siri hiyo ilitolewa na vyombo vya habari vya kijamii vya Nigeria na vilisaidiwa na maoni ya kisiri ya Bi. Buhari.
Filamu yenyewe imerekodiwa katika nyumba ya rais Buhari ya Aso Rock nchini Nigeria.
Je ni nini hiki kinachozungumziwa kuhusu harusi?
Harusi iliopo katikati ya hadithi ambayo ilisambazwa sana katika mitandao ya kijamii inamuhusu rais Muhammadu Buhari na mmoja wa mawaziri wake Bi Sadiya Farouq.
Kile tunachojua ni kwamba rais Buhari amemuoa Aisha Buhari na hajasema chochote kuhusu kuoa mke mwengine mpya.
Bi Farouq naye hajasema chochote kuhusu ndoa hiyo inayozungumziwa.
Ingekuwa rahisi kudai kwamba zilikuwa habari bandia na kuachia hapo , hadi bi Buhari alipotoa tamko.
Je Aisha Buhari alisema nini?
Alikuwa nje ya taifa hilo kwa takriban miezi miwili ambapo alizuru nchini Uingereza ili kufanyiwa matibabu.
Kurudi kwake kulionekana na wale ambao wamekuwa wakifuatilia hadithi hiyo kama njia ya kutetea ndoa yake.
Jibu lake alipoulizwa katika uwanja wa ndege kuhusu harusi halikufutilia mbali uvumi kwamba rais huyo alikuwa anaoa mke mwengine.
Katika mahojiano na BBC Hausa , Mke huyo wa kwanza alithibitisha ijapokuwa kwa njia ya siri , kwamba ni kweli kumekuwa na mipango ya rais Buhari kuoa mke wa pili.
Pia alisema kwamba mke aliyetarajiwa alishangazwa kwa nini harusi haikufanyika. Bi Buhari alisema: Mtu aliyemuahidi kumuoa hakujua kwamba harusi hiyo haitafanyika .
Hakuamini hakuna ndoa hiyo hadi siku ilipopita. Alizungumza kwa lugha ya Hausa , akipima maneno yake bila kutaja majina.
Lakini ilikuwa wazi kutoka kwa mahojiano hayo kwamba bi Buhari alikasirishwa kwamba bi Farouq hakukana uvumi kuhusu harusi hiyo.
Na ili kuchafua mambo zaidi, akaunti ya twitter ya waziri huyo ilikana kuzungumzia kuhusu uvumi huo , ikikana madai yaliotolewa na akaunti bandia yenye jina lake ambayo ilikuwa imekana hadithi hiyo.
Akaunti hiyo ilituma ujumbe ikisema: Nimegundua kwamba kuna akaunti bandia ilio na jina langu@ Sadiya_Farouq_Farouq.
Ningependa kuwaelezea wafuasi wangu kutotilia maanani yaliopo katika akaunti hiyo na habari zozote zilizochapishwa akiongezea kwamba akaunti yake rasmi ni@Sadiya_farouq".
Je Sadiya Farouq ni nani?
Akiwa na umri wa miaka 45 ni mmoja wa mawaziri wachanga katika baraza la mawaziri la rais Buhari , na anaongoza wizara mpya ya maswala ya kibinaadamu , kukabiliana na majanga na maendeleo ya kijamii.
Ni machache yaliojulikana kumhusu kabla ya kupewa wadhfa huo na bwana Buhari mwezi Agosti ili kuongoza .
Kubuniwa kwa wizara hiyo mpya na uteuzi wake uliwashangaza wengi , lakini wale wanaomjua wanasema amekuwa mfuasi mkubwa wa rais huyo kwa miongo kadhaa.
Alikuwa kiongozi wa tume ya taifa ya wakimbizi, wahamiaji na watu walioachwa bila makap IDPS mbali na kuwa mwanachama wa baraza la kampeni la chama tawala cha All Progressives Congress (APC), ambapo alikuwa akisimamia mipango ya uchaguzi , uchunguzi, operesheni na ukusanyaji wa fedha za ufadhili.
Je harusi ilifanyika?
Hapana.
Harusi ilitarajiwa kufanyika ijumaa iliopita, tarehe 11 mwezi Oktoba lakini akunti ya twitter ya Sadiya_ Farouq ilionyesha kuwa alikuwa Uswizi mjini Geneva kutokea siku ya Alhamisi , akiongoza ujumbe wa Nigeria katika mkutano wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa.
Hakurudi Nigeria hadi siku ya Jumanne , kulingana na kile alichochapisha katika akunti yake.
Lakini hakuwazuia watumiaji wa mitandao ya kigeni nchini Nigeria hususan wale wa twitter kutotoa orodha ya wageni waalikwa , eneo la harusi na burudani. Mfuasi huyo wa Twitter alibuni kadi yake ya harusi:
Harusi ya Nigeria haikamiliki bila nguo yenye rangi kwa jina aso-ebi, inayovaliwa na marafiki wa karibu na watu wa familia siku hiyo.
Jamaa huyo aliweka picha ya zamani isio na uhusiano wowote na harusi hiyo.
Je ni nini kinachogombaniwa katika familia hiyo?
Mbali na harusi hiyo bandia kuna mgogoro kati ya ndugu tofauti wa familia kubwa ya Buhari.
Sasa tunajua kufuatia mahojiano hayo ya BBC Hausa kwamba kanda ya video iliosambaa sana katika mitandao ya kijamii ya Aisha Buhari ilikuwa ya kweli.
Alithibitisha kule ilikotoka akisema kwamba ilirekodiwa na nduguye rais ambaye anaishi katika jumba la Aso Rock mwaka 2018.
Bi Buhari anasema kwamba kanda hiyo ya video ilichukuliwa na Fatima Daura, mwanawe Mamman Daura.
Ni mpwa wa Buhari na amekuwa mtu wa karibu wa rais. Hana wadhfa wowote katika serikali lakini anaaminika kuwa na ushawishi mkubwa serikalini.
Alipewa jumba moja - Kwa jina Glass House- katika jumba la rais ambapo kisanga hicho kilitokea katika kanda ya video.
Kulingana na BI Hbuhari : walichukua kanda hiyo mbele ya mlinzi wake na kila mtu aliyekuwepo.. Yeye fatima Daura alikuwa akichukua video hiyo mbele yangu na alikuwa akicheka na kunikejeli.
Walifanya hivyo kwa kuwa mume wangu aliwaondoa kutoka katika nyumba. Aliuwaambia kuchukua mizigo yao na kumwachia mwanawe nyumba hiyo kuishi.
Fatima Daura amejibu mahojiano hayo ya Bi Buhari akisema: Iwapo mtu atafikiria vizuri hawezi kusema kwamba mke wa rais anazuiwa kuingia katika nyumba yake.
Rais wa Nigeria bado hajatoa tamko lolote kuhsu kanda hiyo lakini sikju ya Jumatano, bi Buhari baadaye alichapisha akiomba msamaha katika mtandao wa Instagram, akisema: Natumia fursa hii kuomba msamaha kwa aibu ambayo nimewawekea watoto wangu, ndugu zangu , raia wa Nigeria na taasisi ninayowakilisha katika kanda ya video iliosambaa.".
Aisha Buhari hakusema ni nani aliyekuwa anapanga harusi, lakini ni wazi anajua nani anayepanga.
Baadhi ya watu wanasambaza uvumi kwamba kukataa kwake kuthibitisha chanzo cha kanda hiyo mwaka 2018 , ambapo alimtaja Mamman Daura na mwanawe fatima , ilikuwa ujumbe mwengine wa siri.
Bi Daura anakana kwamba harusi ilikuwa inapangwa , akiambia BBC Hausa kwamba babake na rais ni wanaume waliooa wake mmoja mmoja .
Pia anasema kwamba uwezo na ushawishi ambao unatajwa kuwa na babake unaweza kutoka kwa Mungu pekee.
Je harusi bado ipo?
Hilo litategemea iwapo ilikuwa ikiandaliwa kweli. Kama kuna watu waliokuwa wakipanga basi huenda mipango hiyo haijafutiliwa mbali
Iwapo kuna mtu yeyote ambaye anajua ishara za harusi, basi ni bi Buhari. Alifunga ndoa na rais alipoachana na mkewe wa kwanza 1988.
Rais huyo anajulikana kupenda mke mmoja licha ya kuwa Muislamu ambapo anaruhusiwa kuoa hadi wake wanne.
Bi Buhari alikuwa akizungumzia bi Farouq kama mke aliyetarajiwa katika mahijiano na BBC Hausa na suala kwamba rais wala waziri huyo hawajatoa tamko lolote kuhusu uvumi huo wa harusi , linawafanya wengi kujihisi kana kwamba wanatazama filamu ya ukweli , ama hii hadithi pengine itaendelea.