Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Brexit: Mpango una maana gani? na je utapita bungeni?
Mpango wa Brexit umefikiwa baina ya Uingereza na Umoja wa Ulaya, lakini una maana gani?
Tunajibu baadhi ya masuali makuu yanayoibuka kuhusiana na mambo yalipofikia.
Iwapo bunge halitaupitisha mpango, Je Boris Johnson ataweza kuomba muda wa ziada?
Kwa mujibu wa sheria, ndio anaweza.
Muswada uliopitishwa mwezi uliopita bungeni 'Benn Act', unasema kuwa Johnson atahitajika kuomba kucheleweshwa kwa Brexit kwa miezi mitatu ya ziada - na hiyo ni iwapo tu hatofanikiwa kupitisha muswada, au kuwashawishi wabunge kuidhinisha kujitoa bila ya mpango kufikia Oktoba 19. Jumamosi hii.
Bunge litakuwa na kikao siku hiyo ambapo ndio wabunge wanatarajiwa kupiga kura kukubali au kukataa mpango mpya wa Johnson.
Fahamu zaidi kuhusu Brexit:
Kwa mujibu wa mpango huu, je kutakuwa na mpaka nchini Ireland?
Hapana, hakutokuwana mpaka. Pande zote zimeondosha uwezekano wa kuwepo ukaguzi wa mpakani kati ya Ireland kaskazini na Jamhuri ya Ireland.
Pendekezo la Johnso kwamba huenda kukawa na ukaguzi katika maeneo yalitengwa kutoka mpakani limepingwa na EU.
Matokeo yake, kutahitajika kuwana ukaguzi ndani ya Uingereza kwenyewe, bandarini katika bahari baina ya Great Britain na Ireland kaskazini.
Je Uingereza bado inahitajika kulipa 'ada ya talaka'?
Ndio Uingereza bado itahitajika kuilipa 'ada ya talaka' ya £39bn chini ya mpango wa waziri mkuu Johnson.
Hatahivyo, Kwasababu Uingereza imekaa muda wa ziada ndani ya ada hiyo sasa ni kima cha £33bn.
Mapendekezo mapya yanakaribiana kwa usawa na ya mpango wa waziri mkuu aliyekuwepo Theresa May. Tofauti kuu ni kuhusu suala muhimu la mpaka wa Ireland na iwapo Uingereza itajitoa katika muungano wa forodha kikamilifu baad aya muda kumalizika.
Je safari za kwenda Uingereza zitabadilika baada ya Brexit?
Uingereza haipangi kuidhinisha visa kwa watalii kutoka Umoja wa Ulaya.
kwahivyo, kwa zaiara za muda mfupi, huenda hali isibadilike sana.
Safari zitakuwana gharama kubwa zaidi baada ya Brexit?
Tangu Uingereza ipige kura kujitoa katika EU, thamani ya pauni imeshuka. Hii ni licha ya kukuwa kwa kiasi kidogo baada ya mpango huu mpya kutangazwa.
Hii ni kutokana na wasiwasi mwingi uliokuwepo kuhusu hali itakuwaje wakati Brexit itaidhinishwa.
Ni vigumu kubashiri namna thamani ya sarafu ya pauni itakavyobadilika. Pendekezo moja litakaloweza kukusaidia, ni kwamba ubadili nusu ya pesa zako angalau wiki kadhaa kabla ya safari na nusu ya pili siku chache kabla ya safari.
Je mpango wa Brexit unaweza kuidhinishwa pasi idhiniya bunge la wawakilishi?
Hapana, haiwezekani kwa namna sheria ilivyo sasa.
Sheria ya Umoja wa Ulaya (ya kujitoa) ya mwaka 2018 inasema ili kufikiwa makubalino ya kujitoa ni lazima yaidhinishwe na bunge.
Mpango huu unaruhusu Uingereza kufanya biashara huru na mataifa mengine duniani?
Ndio, Uingereza itajita katika muungano wa forodha na EU, ambapo ndilo jukwaa linalotumika kujadili masuala ya kibiashara kwa mataifa yote wanachama.
Hioy inamaanisha Uingereza itaweza kufikia makubaliano yake binfasi ya biashara na mataifa yasio katika Umoja wa Ulaya pamoja na yaliomo ndani ya EU - licha ya kwamba huenda hili likachukua muda.
Mpango huo unatarajiwa kudumu kwa muda gani?
Mpango huo unaeleza kwamba mwisho wa kipindi cha mpito ni Desemba 2020 wakati Uingereza itajitoa katika taasisi zote za EU, Ireland kaskazini itabidi isalie kufuata baadhi ya sheria za EU. Katika hali fulani itabidi itoze kodi ya EU kwa aina fulani ya bidhaa.
Hali itaendelea mpaka makubaliano mapya ya kuhusu uhusiano wa siku zijazo yatakapofikiwa, au Ireland kaskazini ipige kura kupinga mpango huo. Serikali yake itakuwa na fursa ya kupigia kura vipengee vya mpango huu baada ya miaka minne, halafu kila baada ya angalau miaka minane baada ya hapo.