Ron Ely: Mke wa nyota aliyeigiza Tarzan auawa na mtoto wao

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkewe Ron Ely, nyota wa makala iliyopeperushwa kwenye televisheni miaka ya 60 'Tarzan' amechomwa kisu hadi kufariki na mtoto wao wa kiume nyumbain kwao California Jumanne jioni, Polisi wanasema.
Maafisa walioitwa katika nyumba hiyo ilio kwenye mtaa wa kifahari wa Santa Barbara walimpata Valerie Lundeen Ely, mwenye umri wa miaka 62, akiwa amefariki huku akiwa ana "majeraha kadhaa ya kuchomwa na kisu".
Maafisa wanasema polisi walimzingira Cameron Ely mwenye umri wa miaka 30 nje ya makaazi yao, na kumpiga risasi hadi kufa kutokana na kumchukulia kuwa tishio.
Hapakuwa na taarifa ya iwapo muigizaji mkongwe Ely mwenye umri wa miaka 81 alijeruhiwa wakati wa shambulio hilo.

Chanzo cha picha, Silver Screen Collection
Lakini hapo awali ofisi ya mkuu wa polisi ilieleza kuwa mwanamume mtu mzima mlemavu aliyekuwepo ndani ya nyumba hiyo amepelekwa hospitalini kufanyiwa ukaguzi.
Taarifa ya hivi punde ya idara hiyo ya polisi Santa Barbara imesema: "Maafisa waliipekuwa nyumba na maeneo ya karibu kumtafuta Cameron Ely.
"Wakati wa upekuzi huo, mtuhumiwa alipatikana nje ya nyumba.
"Alikuwa tishio maafisa wannne walimfyetulia silaha mshukiwa na kumuua."

Chanzo cha picha, Silver Screen Collection
Ron Ely anafahamika pakubwa kwa kuigiza kipindi cha Tarazan kilichopeperushwa kati ya 1966-68.
Tarzan alikuwa ni mshiriki katika kipindi hicho aliyelelewa na nyani katika jangwa la Afrika, katika kitabu cha Edgar Rice Burroughs kilichochapishwa mnamo 1914.
Ely apia aliigiza kama muigizaji mkuu katika filamu ya mnamo 1975 Doc Savage: The Man of Bronze.
Taarifa kuu leo:
Bi Lundeen alikuwa mlimbwende aliyeshinda taji la Miss Florida.
Wawili hao wana mabinti wawili pia, Kirsten and Kaitland.
Ron Ely alipumzika uigizaji kati ya 2001-14 kabla ya kurudi na kushiriki katika filamu 'Expecting Amish'.

Chanzo cha picha, Tibrina Hobson/Getty Images
Ameliambia jarida la Charlotte Observer wakati filamu hiyo ilipotoka kwamba: "NIlisitisha uigizaji kuilea familia yangu na kuoata fursa ya kukaa nao zaidi hapa Santa Barbara.
Muigizaji huyo pia aliandika vitabu viwili, Night Shadows, mnamo 1994, na East Beach, alichokiandika mwaka mmoja baadaye.













