Papa Francis amtangaza kadinari Newman kuwa mtakatifu mpya

papa

Chanzo cha picha, Getty Images

Kadinari John Henry Newman ametangazwa kuwa mtakatifu na kanisa katoliki, katika maadhimisho ya misa iliyoongozwa na papa Francis hii leo huko Rome, Italia.

Misa ya wazi ilihudhuriwa na maelfu ya watu waliokuja kwenye hija.

Kadinari Newman, ambaye alifariki huko Birmingham mwaka 1890, ni muingereza wa kwanza kutangazwa kuwa mtakatifu kwa kipindi cha takribani miaka 50.

Mwana mfalme Wales alijumuika katika misa hiyo ambayo ilikuwa inawatambua wanawake wengine wanne kuwa watakatifu.

Pope Francis leading the Mass

Chanzo cha picha, REUTERS/Remo Casilli

Maelezo ya picha, Papa Francis akiongoza misa takatifu katika makutano ya kanisa la Mt. Peter, Rome, maelfu ya watu walihudhuria
Prince Charles at the service

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Prince Wales ahudhuria sherehe za kumtangaza kadinari John Henry Newman kuwa mtakatifu kwa karne ya 19

Mama Mariam Thresia kutoka India, Marguerite Bays kutoka Uswizi, Mama Giuseppina Vannini kutoka Italia na sista aliyezaliwa Brazili Dulce Lopes Pontes walikuwa wanatambuliwa pia kuwa watakatifu katika misa hiyo.

John Henry Newman

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtakatifu John Henry Newman ni muingereza wa kwanza kutambulishwa tangu mwaka 1970

Maelfu ya waingereza walisafiri mpaka Rome ili kusheherekea utambulisho huo.

Carol Parkinson, katibu wa marafiki wa Newman kutoka mji wa Birmingham, anasema kuwa kutangazwa kwa mtakatifu huyo ni kwa kipekee na imekuwa siku ya hisia kubwa kwao.

"Uadilifu wake, urafiki wake, uaminifu pamoja na bidii aliyoweka katika kazi yake ni mfano mzuri wa kuigwa na kila mtu", alisema.

A priest giving instructions at the Vatican

Chanzo cha picha, Reuters

Kadinali Newman alizaliwa mjini London mwaka 1801, alisoma chuo cha Trinity College na Oxford.

Alikuwa anatarajiwa kuwa padri wa kianglikana lakini alibadili dini na kuwa mkatoliki mwaka 1845.

Newman amesifika kwa miujiza miwili , muujiza wa kwanza ni kumponya mgonjwa wa uti wa mgongo wa kium na kumponya mwanamke aliyekuwa aachi kutokwa damu.

Pope Francis and clergyman

Chanzo cha picha, Reuters

Presentational grey line