Tetesi za soka Ulaya Jumapili 13.10.2019: Eriksen, Defoe, Rice, Kane, Rashford, Fernandinho

Bayern Munich inaweza kushindana na Real Madrid katika harakati za kumsainisha kiungo wa Tottenham Hotspur, mchezaji wa Denmark mwenye umri wa miaka 27, Christian Eriksen mnamo Januari.
(Sport1, via Sunday Mirror)
Steven Gerrard Bossi wa Ranger anasema mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Jermain Defoe - amabe yupo kwa mkopo huko Ibrox kutoka Bournemouth - anaweza kupewa jukumu la ukocha mchezaji kwenye klabu ya Scottish Premier msimu ujao. (Daily Record)

Manchester United inatarajiwa kuwa na hadi pauni milioni 300 kwaajiki ya kutumia misimu ijayo - lakini Nahodha wa zamani wa timu hiyo Bryan Robson anasema ilikuwa ni makosa kupoteza majina makubwa akiwemo mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, na Chile Alexis Sanchez, 30, hawakuwatafutia mbadala.(Daily Star Sunday)
Wolves wanahusishwa na mlinzi wa Galatasaray kutoka DR Congo Christian Luyindama, 25 - ikumbukwe Luyindama alikuwa katika mipango ya Aston Villa. (Birmingham Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Waingereza wawili wa timu ya taifa - Spurs 'Harry Kane, 26, na Marcus Rashford wa Manchester United, 21 wako kwenye orodha ya mabingwa wa Uhispania Barcelona. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Manchester City mwenye umri wa miaka 34, Fernandinho, mkataba wake unafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu, yuko kwenye mpango mpya wa kuongeza mkataba wa miezi 12 kwenye Uwanja wa Etihad. (Sun on Sunday)


Mkuu wa United Ole Gunnar Solskjaer anataka kilabu cha Manchester United kutumia huduma ya ushauri kutoka chini Uhispania ili kusaidia katika kuajiri.(Mail on Sunday)
Manchester United inampango wa kutumia pauni milioni 70 kusaini kiungo wa West Ham United ya London, Deslan Rice, 20, mnamo Januari. (Sunday Mirror)

Kipa wa wagonga nyundo wa London West Ham, Lukasz Fabianski, 34, anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi mitatu baada ya upasuaji kwenye jeraha lake la paja.(London Evening Standard)
Newcastle United wanafuatilia kiungo wa Queens Park Ranger 'wa Ireland Ryan Manning, 23. (Football Insider)
Afisa wa zamani wa Bolton Wanderers Phil Parkinson ndiye mgombea anayeongoza kuwa meneja mpya wa League One upande wa Sunderland.(Daily Star Sunday)

Timu ya Newcastle wana mpango wa kumsaidia meneja wao Steve Bruce Kipindi cha Dirisha dogo la usajiri hapo Januari mwakani mipango hiyo imeshaanza kufanyiwa kazi katika ofisi za St. James' Park.(Newcastle Chronicle)
Kocha Mkuu wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Sven-Goran Eriksson anasema kuwa bado anajitahidi kukabiliana na sehemu ambayo vyombo vya habari vilicheza katika kufukuzwa kwake kwenye timu ya taifa.(Sunday Times - subscription required)













