Kwa picha: Historia ya jamii ya Wakrio wa Sierra Leone

An African Minister Administering the Sacrament

Chanzo cha picha, Museum of London

Presentational white space

Watu wa kabila la Krio nchini Sierra Leone walitokana na kizazi cha watumwa wa kiafrika waliowapigania waingereza katika vita vya uhuru vya Marekani, mara baada ya kuahidiwa uhuru wao.

Baada ya Marekani kushinda vita hivyo 1783, walitoroka pamoja na wanajeshi wa Uingereza hadi Canada, ambako walisafirishwa na kurudishwa Afrika katika koloni la Uingereza la Sierra Leone.

Koloni hilo lilibuniwa kuwapa makazi watumwa walioachiliwa huru hata kabla ya biashara ya watumwa kupigwa marufuku mwaka 1807.

Baadhi ya wanaharakati wakuu wa Uingereza waliotaka utumwa kufutiliwa mbali walikua na matumaini kuwa watumwa walioachiliwa wameathiriwa na utamaduni wa Uingereza na Ukristo na kwamba wangelisambaza utamaduni huo katika eneo lote la Afrika Magharibi.

Leo, Wakrio wanakadiria 2% ya idadi ya watu nchini Sierra Leone.

Muonekano wao ni tofauti japo ingawa mtindo wao wa maisha umechangiwa pakubwa na ushawishi wa Uingereza.

Lugha ya Kikrio, inazungumzwa na watu wengi nchini Sierra Leone na imetokana na msingi wa Kiingereza, pamoja na lugha mbali mbali za Kiafrika.

Maonyesho ya "The Krios of Sierra Leone"yanayoandaliwa na makavazi ya Dockland mjini London, kuangazia mavazi ya jamii hiyo na utamaduni na mtindo wao wa maishi.

Plan of the Colony of Sierra Leone 1825

Chanzo cha picha, Museum of London

Presentational white space

Ramani hiyo hapo juu ilichorwa na afisa wa jeshi la Uingererza mwaka 1825 na inajumuisha vijiji vilivyobuniwa na watu ambao baadaye walifamika kama Wakrio.

Interior of a Girls School

Chanzo cha picha, Museum of London

Presentational white space

Magavana wa Uingereza walioongoza Sierra Leone walihakikisha wageni waliofika katika koloni hilo walifuata utamaduni wa wakristo wa Uingereza.

Waliwatumia wamishonari kujenga makanisa na mashule wakiwa na lengo kuwa wakaazi wa eneo hilo wanakuwa waalimu, wachungaji na wamishonari katika kanda nzima ya Afrika Magharibi.

Picha unayoina hapo juu inaonesha shule ya wasichana ambayo bado inatumika hadi wa leo na imesalia kuwa shule ya kifahari nchini Sierra Leone.

Krio dress

Chanzo cha picha, Museum of London

Presentational white space

Nguo hii huvaliwa na wanawake wa Krio. Ina mikoni mirefu, mshipi nakamisi inayovaliwa chini yake.

Huvaliwa pamoja na mkoba na kikoi.

Kapet slipas

Chanzo cha picha, Private collection of Iyamide Thomas

Presentational white space

Pampu hizi za "Victoria" pia zilikua maarifu. Michoro iliyotumika inafahamika kama "marking carpet".

Mtindo huu unaitwa "wingu", huku mitindo mingine ikijumuisha "almasi" na "trellis".

Silver entrée dish presented to Thomas Cole. Object lent by Charles Stuart Dudley Cole

Chanzo cha picha, Charles Stuart Dudley Cole

Presentational white space

Sahani ya fedha ilikabidhiwa kwa Thomas Cole, kaimu waziri wa koloni la Sierra Leone, mwaka 1831.

Alikua na jukumu la kuwakaribisha katika koloni hilo watumwa walioachiliwa huru baada ya kukombolewa katika meli za wafungwa.

Wooden Tillet Block with central panel of ship with the wording Sierra Leone Company (c) Museum of London.jpg

Chanzo cha picha, Museum of London

Presentational white space

Nyumba karibu 1800 za mbao zilitengenezwa na kuwekwa nembo ya kampuni ya Sierra Leone .

Kampuni hiyo iliifanya Sierra Leone kuwa koloni yake mwaka 1792, lakini baadaye ikafilisika na ndipo serikali ya Uingereza kuchukua uongozi yake.

Nchi hiyo ilikuwa koloni rasmi ya Uingereza mwaka 1808.

Archbishop-Samuel Ajayi-Crowther

Chanzo cha picha, Church Mission Society archives, Oxford

Presentational white space

Samuel Adjai Crowther alizaliwa nchini Nigeria, ambako alizuiliwa na watumwa.

Meli ya vita ya Uingereza alikamata meli ya watumwa ambayo ilitumiwa kumsafirisha hadi Freetown kama"mkombozi wa Waafrika" akiwa na karibu miaka 13 .

Crowther alikua mwanafunzi wa kwanza wa Taasisi ya Fourah Bay. Alitawazwa kuwa kasisi nchini Uingereza mwaka 1843 na kuwa kasisi wa kwanza mwafrika wa wa kanisa la kianglikana mwaka 1864.

Pia anafahamika kwa kutafsiri Bibilia takatifu katika lugha ya Kiyoruba, ambayo ni moja ya lugha kuu inayotumiwa nchini Nigeria.

Bunce Island

Chanzo cha picha, Peter C Andersen

Presentational white space

Uingereza iliingia kijeshi Sierra Leone kwa mara ya kwanza miaka ya 1670.

Ilikua ya kwanza kukalia kisiwa cha Bunce na kutumia mto wa Sierra Leone kusafirisha kufanya biashara.

Kabla ya sheria ya mwaka 1807 kupiga marufuku biashara ya watumwa, kisiwa cha Bunce kilifahamika kama "kiwanda cha watumwa"na maelfu ya watu kutoka Afrika magharibi walizuiliwa hapo na kusafirishwa katika mataifa ya ulaya na Marekani.

Presentational white space
Johnny Smythe

Chanzo cha picha, Museum of London

Presentational white space

John Henry Smythe alizaliwa mjini Freetown na alihudumu katika jeshi la Sierra Leone.

Baada ya kutangazwa vita mwaka 1939, alijitolea kuhudumu katika jeshi la angani la Uingereza (RAF), na kupewa mafunzo ya kama afisa wa majini.

Mwaka mmoja baadaye alikua msimamizi wa kikosi cha mabomu kabla ya kupandishwa kuwa afisa wa kuruka.

Smythe alihudumu katika kikosi cha 27 cha walipuaji mabomu wa RAF katika mataifa ya Ujerumani na Italia.

Mwaka 1943 alipelekwa gerezani baada ya kupigwa risasi na wapigaji maadaui.

Alizuiliwa katika kambi ya wafungwa nchini Ujerumani kwa miezi 18 hadi kambi hiyo ilipo kombolewa na Urusi mwaka 1945.

Vita vilipomalizika, Smythe alisaidia kuwashawishi wanaume wa India Mashariki kutoondoka katika dola hilo na baadae akateuliwa kuwa mwakilishi maalum wa watu hao katika mahakama ya Uingereza.

American Wooden houses

Chanzo cha picha, Melbourne Garber

Presentational white space

Nyumba hizi zilizo katika ufuo wa bahari mashariki mwa Marekani zimejengwa kwa misingi ya mawe, zimeigwa nchini Sierra Leone na jamii ya Nova Scotia - watumwa wa zamani waliokimbia pamoja na wanajeshi wa Uingereza baada ya kushindwa katika vita wakati wa mageuzi ya Marekani.

Nyumba hizi zilifahamika kama bod os (nyumba za mbao), kwa lugha ya Krio, ambayo inazungumzwa na watu wengi nchini Sierra Leone.

Baada ya mwaka 1940, ujenzi wa nyumba kama hizo ulipigwa marufuku kutokana na sababu za kiusalama lakini mfumo huo wa ujenzi tayari umepungua baada ya ujenzi wa kutumia mawe kupendelewa na wengi.

Picha zote zina haki miliki.