Mama Maria Nyerere awasili na kupelekwa hospitali kwa matibabu baada ya kuugua Uganda

Mama Maria Nyerere aliugua alipokuwa nchini Uganda kwa ajili ya Ibada maalum ya mashahidi wa Uganda
Maelezo ya picha, Mama Maria Nyerere aliugua alipokuwa nchini Uganda kwa ajili ya Ibada maalum ya mashahidi wa Uganda
    • Author, Na Dinah Gahamanyi
    • Nafasi, BBC Swahili

Mke wa rais wa zamani wa Tanzania Maria Nyerere amewasili jijini Dar es Salaam Tanzania na kupelekwa hospitalini baada ya kupata matatizo ya kiafya nchini Uganda.

Akizungumza na gazeti la The Citizen,nchini humo mtoto wake wa kiume Makongoro Nyerere amesema kuwa kufuatia matatizo ya kiafya aliyoyapata akiwa jijini Kampala, Madaktari wa Tanzania Tanzania walichukua jukumu la kupatia matibabu kabla ya kumruhusu kurejea nchini Tanzania travel back to Tanzania.

"Tunavyoongea sasa, ndio amewasili Dar es Salaam, na kulingana na mapendekezo kutoka kwa madaktari , tunampeleka moja kwa moja hospitalini kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya kuchukua maamuzi yoyote ," alisema Makongoro.

Amesema wanakwenda hospitalini kupata uhakika juu ya ikiwa bado anahitaji kuendela kupata matibabu au yuko katika hali nzuri ya kumuwezesha kurejea nyumbani.

Awali mke huyo wa rais wa zamani wa Tanzania Maria Nyerere amesindikizwa leo na maafisa wa Uganda ambako atapanda ndege kurejea nyumbani baada ya kuugulia nchini Uganda.

Anaondoka kutoka uwanja wa ndege wa Entebbe kwa ndege rasmi aliyopewa na rais wa Uganda Yoweri Museveni hadi mjini Dar es salaam ambako anatarajiwa kuendelea na matibabu zaidi.

Rais Museveni anaripotia kutohudhuria sherehe za siku ya mashahidi wa Uganda katika eneo la Namugongo kwa ajili ya kumtembelea Mama Maria mjini Kampala

katika hospitali mjini Kampala.

Mahujaji katika hekalu la mashahidi wa Uganda

Chanzo cha picha, Uganda Martyrs Catholic shrine/Facebook

Maelezo ya picha, Mahujaji katika hekalu la mashahidi wa Uganda

Duru zinasema kuwa ilibidi rais Museveni kumtuma wawakilishi kwenye tukio la siku ya mashahidi wa Uganda ili kuwaepusha waumini kusubiri kwa muda mrefu , ili aweze kwenda kumuona Mama Maria Nyerere ambaye alikuwa katika hospitali moja mjini Kampala.

Mama Maria Nyerere(kushoto) akiwa pamoja na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Chanzo cha picha, Blogi ya Taifa ya CCM

Maelezo ya picha, Mama Maria Nyerere(kushoto) akiwa pamoja na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Bwana Museveni alisema kuwa hakuna mtu hata mmoja aliyewahi kuwa na mchango mkubwa kwa kipindi cha miaka milioni nne kwa Afrika zaidi ya Mwalimu Julius.

Duru zinasema kuwa Mama Nyerere mwenye umri wa miaka 88, alipata matatizo ya kiafya usiku kabla ya tukio la kumkumbuka mumewe Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Baadhi ya mahujaji katika tukio la kuwakumbuka mashahidi wa Uganda

Chanzo cha picha, Uganda Martyrs Catholic shrine/Facebook

Mwandishi wa BBC mjini Kampala anasema kuwa hali ya kiafya mjane huyo wa musasisi wa taifa la Tanzania imeripotiwa kuendelea kuimarika.

Tangu mwaka 2009, waumini wa kanisa katoliki wamekuwa wakifanya ibada katika hekalu la Namugongo kwa ajili ya kumkumbuka mwalimu Nyerere.

Mama aria Nyerere ambaye ni mke wa rais wa zamani wa Tanzania alikuwa nchini Uganda kwa ajili ya ibada maalum ya kukumbuka mchango wa hayati Mwalimu juliasi Nyerere kwa Afrika na Ukristo.

Juni Mosi, rais Yoweri Museveni wa Uganda na Mama Maria Nyerere walishiriki pamoja ibada hiyo maalumu iliyofanyika katika hekali la mashahidi wa Uganda la Namugongo.

Nyerere alitoa mchango wa zana kuwasaidia waasi wa Bwana Museveni kwa ajili ya kuung'oa madarakani utawala wa rais Idi Amin.

Bibi amekuwa akisafiri kwenda hadi Namugongo Uganda kwa miaka 13 mfulurizo kwa ajili ya sherehe za kuwakumbuka mashahidi wa Uganda.