Pundamilia 'alibino' apatikana mbuga ya wanyama pori Masai Mara Kenya

Punda milia

Chanzo cha picha, Royal Media Kenya

Muda wa kusoma: Dakika 1

Pundamilia mwengine mwenye ngozi ya kipekee ameonekana katika mbuga ya wanyama pori ya Masai Mara nchini Kenya.

Picha zimeonyesha kwamba pundamilia huyo ana ishara kama za alibino , mistari ya myeupe na myeusi inaonekana katika shingo na miguu.

Ripoti zinasema kwamba punda milia huyo amepewa jina la Manie baada ya mwelekezi wa safari kwa jina John Manie KiIpas aliyemuona kwa mara ya kwanza.

Katika mitandao ya kijamii Emmanuel Kibitok alisema: kuna mtu anawapaka rangi pundamilia katika mbuga ya Masai Mara. Wapakaji rangi katika mbuga ya masai mara wameshkwa na wazimu.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Katika mitandao ya kijamii Gitweeta alichapisha picha ya hivi karibuni pamoja na ile ya Tira, pundamilia asiye wa kawaida mwenye madoa meusi ambaye alionekana nchini Tanzania wiki moja baada ya kuondoka katika hifadhi ya wanyama pori ya Maasai Mara .

Tira ambaye alikua na miezi michache tangu azaliwe, aliondoka Kenya na wazazi wake wakati wa uhamiaji wa nyumbu.

Pundamilia huyo alipatiwa jina hilo na Antony Tira, mwelekezi wa safari za watalii na mpiga picha ambaye alimuona mnyama huyo kwa mara ya kwanza katika kambi ya kichakani katika ukurasa wa Facebook.

Ripoti ya jarida la Forbes ilisema kuwa picha hizo ziliwashangaza watalii ambao walipiga simu huku wapenzi wa wanyama wakitaka kumuona mnyama huyo wa ajabu.

Wataalam wanasema kwamba punda milia huyo alidhaniwa kuwa na ugonjwa ambao wanyama huonyesha ulemavu fulani katika mistari yao ya mwilini.