Vita Iraq: Umoja wa mataifa unataka 'mauaji ya watu yasio na maana' yasitishwe

Umoja wa mataifa unataka 'mauaji ya watu yasio na maana' yasitishwe nchini Iraq wakati idadi ya watu waliouawa kutokana na maandamanao ya kuipinga serikali ikikaribia kufika 100.

Waandamanaji wanasema wanachukua msimamo dhidi ya ukosefu wa ajira, huduma mbovu za umma na ufisadi nchini.

Jeanine Hennis-Plasschaert,mkuu wa kitengo cha ujumbe wa usaidizi kwa Iraq katika Umoja wa mataifa anasema: "Siku tano za mauaji na majeruhi: ni lazima lisitishwe."

Waliohusika na vifo vya watu wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria, amesema.

Hapo jana Jumamosi vikosi vya usalama vilitawanya maandamani ya umma mashariki mwa Baghdad.

watu watano wanaarifiwa kufariki katika mapigano ya hivi karibuni katika mji mkuu.

Vikosi vya usalama vinaripotiwa kwa mara nyingine kutumia risasi za moto na gesi ya kutoa machozi.

Takriban watu 99 wamefariki na wengine karibu 4000 wamejeruhiwa tangu kuanza kwa ghasia katika mji mkuu huo siku ya Jumanne kabl aya kusambaa kusini mwa Iraq, tume ya haki za binaadamu ya bunge la Iraq imesema.

Ni ghasia mbaya kuwahi kushuhudiwa tangu kutangazwa kushindwa kwa kundi la Islamic State nchini humo mnamo 2017.

Inaonekana kama changamoto ya hivi karibuni kwa serikali dhaifu ya waziri mkuu Adel Abdel Mahdi, takriban mwaka mmoja tangu aingien madarakani.

Maafisa wa utawala wamekuwa wakijaribu kudhibiti maandamano hayo kupitia kuidhinishwa marufuku ya kutoka nje na kuzimwa kwa mtandao nchini.

Nini nikanchofanyika hivi sasa?

Marufuku iliyoidhinishwa mchana ya kutotoka nje Baghdad iliondolewa Jumamosi, na makundi madogo ya waandamanaji wakaanza kukusanyika tena.

Midani ya Tahrir ndio sehemu ambapo waandamanaji wanamiminika lakini ilifungwa Jumamosi kwa mujibu wa mashirika ya habari nchini.

Kikao cha dharura cha bunge kilishindwa kuendelea Jumamosi mchana.

Vituo kadhaa vya televisheni vlishambuliwa zikiwemo ofisi za kituo cha habari kinachomilikiwa Saudia - Al-Arabiya.

Huko Nasiriyah, waandamanaji waliteketeza moto makao makuu ya vyama visita tofauti vya kisiasa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, maelfu walimiminika katika makao ya gavana katika mji wa kusini wa Diwaniyah.

Waandamanaji hawaonekani kuwana uongozi wa wazi kwa hivi sasa, na hasira yao inazidi kufanya matakwa yao kuwa makali zaidi anasema mwandishi wa BBC Sebastian Usher.

Kumekuwa na hisia gani?

Siku ya Ijumaa Waziri mkuu Mahdi aliapa kujibu malalamiko ya waandamanaji lakini alionya kwamba hakunu suluhu ya miujiza kwa matatizo ya Iraq.

Amesema ameviunga vikosi vya usalama mkono kikamilifu, akasisitiza wanatii 'viwango vya kimataifa' katika kukabiliana na waandamaji.

Umoja wa mataifa na Marekani zimeelezea wasiwasi kuhusu ghasia, na kuomba maafisa nchini Iraq kujizuia.

Kwanini haya yanafanyika hivi sasa?

Ufisadi, ukosefu wa ajira na huduma duni za umma ni makuu yaliochangia kutoridhishwa kwa vijana wengi Iraq hii leo.

maandamano hayo yalianza ghafla kukiwa hakuna muongozo rasmi katika maeneo mengi ya madhehebu ya Shia kusini na kusambaa haraka.

Iraq ina akiba ya nne kwa ukubwa duniani ya mafuta lakini 22.5% ya idadi ya watu ndhini kati ya watu milioni 40 wanaishi chini ya $1.90 kwa siku mnamo 2014, kwa mujibu wa benki ya dunia.

Kiwango cha ukosefu wa ajira kilikuwa ni 7.9% mwaka jana lakini miongoni mwa vijana kiwango hicho kimeongezeka mara mbili. Na takriban 17% ya vijana wanaochangia uchumi wa nchi wanalipwa malipo duni.

taifa hilo pia linajitahidi kukabiliana na vita vikali dhidi ya IS lililochukua udhibiti wa sehemu kubwa za maeneo ya kaskazini na magharibi mnamo 2014.

Hali ya maisha ni duni katika maenoe mengi yalioathiriwa na mizozo, huku kukiwepo na uhaba wa huduma.