Silaha nzito za jeshi la China zilizowashangaza wataalam wa zana za kijeshi duniani

''Hakuna taifa linaloweza kuzuia hatua zilizopigwa na taifa na raia wa China''.

Rais Xi Jinping aliweka wazi ujumbe wake siku ya Jumanne , tarehe mosi mwezi Oktoba katika maadhimisho ya chama tawala cha kikomyunisti tangu kichukue mamlaka.

China sio tena taifa lililomchukua Mao, lenye umasikini ama taifa lililo na unyonge mkubwa kimataifa.

Xi aliongoza gwaride lake la tano la kijeshi na kubwa zaidi katika historia ya China, katika maonyesho ya uwezo wa kijeshi ambao umeafikiwa na taifa hilo pamoja na chama tawala cha kikomyunisti katika wakati uliojaa changamoto , miongoni mwao Hong Kong, ambapo sherehe hizo zilishirikishwa na ghasia na waandamanaji wanaounga mkono demokrasia tangu jimbo hilo lilipopita katika mikono ya China 1997.

Katika gwaride hilo la kijeshi mjini Beijing lililopangwa kwa maelezo madogo kabisa na kushuhudiwa na makao makuu ya serikali, zaidi ya wanajeshi 15,000 walishiriki na 40% ya silaha zilionyeshwa kwa umma kwa mara ya kwanza, kulingana na vyombo rasmi vya habari.

''Nguvu ya kuafikia ndoto hiyo''

Kama ilivyotarajiwa, China ilizindua ndege moja isio na rubani inayobeba silaha mbali na mfumo wa silaha za kizazi kijacho ambazo ziliwavutia wataalam.

Inawez kubeba hadi vichwa kumi vya Kinyuklia kila mojawapo kikiwa na lengo tofauti kulingana na chombo cha habari cha taifa hilo.

Miongoni mwao ni silaha aina ya Dongfeng 41 ikiwa nguzo ya uwezo wa kinyuklia wa China - silaha ya masafa marefu inayoweza kufika eneo lolote nchini Marekani kati ya kilomita 12000 hadi 15,000.

Inaweza kusafirisha hadi vichwa kumi vya kinyuklia kila moja kikiwa na lengo tofauti kulingana na chombo hicho cha habari.

Sampuli ya kombora hilo la DF-41 ilioonyeshwa ni ujumbe kwa ulimwengu kwamba China ina uwezo wa kutosha wa kinyuklia na kwamba iko tayari kimkakati kukabiliana na magendo yoyote kutoka taifa jingine , lilisema gazeti rasmi The Global Times ikiwanukuu wataalam wa Kijeshi.

Sherehe hiyo pia ililionyesha kombora jingine la masafa marefu kwa jina DF-17 ambalo linashirikisha gari linaloweza kubeba nyuklia na mizigo ya kawaida.

Aina hiyo ya silaha ambayo wataalam wanailinganisha na mfumo wa Urusi wa Avangard ina uwezo wa kukwepa mifumo ya kutungua makombora.

Silaha ya DF-17 ilizinduliwa mbele ya umati ulioshuhudia gwaride hilo ikiwa imebeba kombora kulingana na vyombo vya habari.

Baadhi ya wataalam waliozungumza na vyombo vya habari vya Marekani walisema kwamba ni silaha ya kipekee ambayo mataifa ya magharibi hayawahi kuunda.

Katika runinga ya China ya CCTV , watangazaji waliielezea kwamba zana za silaha za China zina nguvu ya kuafikia ndoto ya taifa na jeshi lenye uwezo mkubwa.

Katika maadhimisho hayo , pia walionyesha silaha aina ya JL-2 , zilizo na uwezo wa kurushwa kutoka kwa manuwari zikiwa na umbali wa kilomita 7000 mbali na ndege isio na rubani kwa jina Gongji-11 (GJ-11), ilio na uwezo wa kushambulia eneo bila kuonekana.

Maonyesho hayo yalibaini kwamba Gonji tayari imekuwa ikitumiwa na jeshi la China kulingana na mtandao wa Twitter wa jarida la Global Times.

Mbali na ndege hiyo isio na rubani ni ile ya DR - 8 ambayo imeanza kutumika, kama inayoelezewa na gazeti la Hong Kong , The South China Morning Post.

Ndege hiyo isio na rubani aina ya DR- 8 inaweza kuchukua jukumu muhimu iwapo kutatokea mgogoro dhidi ya meli ya Marekani inayobeba ndege za kijeshi katika bahari ya Pacific ama hata kusini mwa bahari ya China.

Katika maadhimisho hayo, toleo jipya la kombora la kimkakati la China kwa jina, H6-N, ambalo litaweza kusafirisha silaha za atomiki kwa umbali mkubwa kuliko watangulizi wake pia lilionyeshwa , kulingana na AFP.

Silaha hiyo mpya inaweza kubeba makombora katika mbawa zake ikiwa na uwezo wa kusafiri kwa umbali wa kilomita 2000.

Hatua hiyo inamaanisha inaweza kushambulia Alaska, Guam, Hawaii, Malaysia, Ufilipino , Vietnam hata Moscow bila ya kutoka katika anga ya China , kulingana na gazeti la South China Morning Post.

Hatua kubwa zilizopigwa

Jeshi la Peoples Liberation la China lilisisitiza kwamba gwaride hilo litaonyesha hatua lilizopiga katika maswala ya kiteknolojia na watalaam kadhaa walikiri kuona hatua hizo.

Ujumbe muhimu wa gwaride hilo la kijeshi ni kwamba limeingia katika enzi mpya, ile ya Xi Jinping, alisema Alezander Neil mtafiti mkuu katika taasisi ya mafunzo ya kimkakati katika eneo la Asia Pacific katika chapisho jipya la BBC.

Rais Xi Jinping alifanya mabadiliko muhimu katika sekta hiyo 2015 kwa lengo la kulifanya jeshi hilo kuwa la kisasa.

Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, bajeti ya ulinzi iliongezeka kwa asilimia 10 kila mwaka na kwa sasa imefikia dola bilioni 168.2 ambayo inaifanya China kuwa taifa la pili kwa matumizi ya kuboresha jeshi lake baada ya Marekani.

Hatahivyo , taifa hilo limepunguza matumizi yake katika sekta hiyo na kusema kwamba hiyo inatokana na tofuti kubwa iliopo na Marekani ambayo matumizi yake yamefikia dola bilioni 643.3 mwaka 2018.

''Baada ya mabadiliko hayo makubwa, jeshi la China lipo katika nafasi nzuri kuelekea katika kuwa jeshi la kisasa kufikia 2035 na la kwanza kufikia 2018'', alisema Neil.

''Hatahivyo, ijapokuwa gwaride hilo linaweza kuonyesha kiwango cha uwekezaji wa jeshi la China, haliwezi kuonyesha uwezo wote wa kijeshi wa taifa hilo, alisema kabla ya sherehe hiyo''.

''Jeshi la China lipo nyuma kwa miongo kadhaa kufikia uwezo wa kijeshi wa Marekani''.