Mateka wa Iran aachiliwa na maharamia wa kisomali baada ya miaka minne

Freed sailor

Chanzo cha picha, .

Maelezo ya picha, Mohammad Sharif Panahandeh alitekwa na maharamia mwaka 2015

Baharia raia wa Iran amechiliwa na maharamia wa Kisomali baada ya kumteka kwa zaidi ya miaka minne.

Mohammad Sharif Panahandeh alikuwa "mgonjwa sana " na ameachiliwa kwa sababu za kibinadamu , limesema shirika linalowasaidia waliotekwa nyara (HSP),ambalo ndilo lililosaidia katika juhudi za kuachiliwa huru kwake.

Kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita, maelfu ya wafanyakazi wa baharini wamekuwa wakitekwa nyara kwenye mwambao wa Somalia na kuachiliwa huru baada ya kulipa kikombozi.

Kuachiliwa huru kwa Bwana Sharif kunamaanisha kuwa maharamia wanawashikilia mateka sasa watu watatu tu.

Mashambulio ya uharamia katika kanda hiyo yaliongezeka mnamo mwaka 2011 lakini yakapungua hadi miaka ya hivi karibuni , kulingana na kikosi cha wanamaji cha Ulaya ambacho kinaendesha shughuli zake katika eneo hilo .

Chati
Maelezo ya picha, Chati inayoonyesha mashambulio ya uharamia nchini Somalia kati ya mwaka 2008 hadi 2018

Mateka watatu waliosalia wote ni raia wa Iran na walichukuliwa pamoja na Bwana Sharif kutoka kwenye boti ya uvuvi mwezi Machi 2015, John Steed kutoka HSP aliiambia BBC.

" Bwana Sharif ana utapiamlo wa kiwango cha juu. Amepoteza uzito mkubwa wa mwili na ana matatizo makubwa ya tumbo na anavuja ndani ya mwili wake ," Bwana Steed amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema.

Baharia huyo amepelekwa katika mji mkuu wa Ethiopia Adis Ababa , kwa ajili ya matibabu ya mwanzo, na anatarajiwa kusafirishwa kwa ndege hari nyumbani Iran.

Map showing location of Ethiopia and Somalia

Iran imeushukuru Umoja wa Mataifa , shirika la HSP, na mamlaka katika jimbo lililojitenga na somalia la Puntland rpamoja na Ethiopia kwa usaidizi , kulingana na taarifa za shirika la habari la Reuters ambalo limewanukuu maafisa wa Iran.

Bwana Sharif aliachiliwa huru kwasababu ya afya yake , lakini maharamia huenda bado watataka walipwe kikombozi kwa ajili ya mateka watatu waliosalia , Bwana Steed ameliambia shirika la AFP.

Kupungua kwa uharamia katika maeneo ya fukwe za Somalia kumetokana na matumizi ya walinzi wenye silaha wanaopiga doriabaharini dani ya meli, wakiwemo wanajeshi kadhaa wa vikosi vya majini kutoka Muungano wa Ulaya na Nato.

Unaweza pia kusikiliza:

Maelezo ya sauti, Sababu ya visa vya uharamia kuanza kuongezeka Somalia