Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ni kwanini wanasiasa wa Korea Kusini wananyoa vichwa ?
Viongozi wa upinzani nchini Korea Kusini wamekuwa wanasiasa wa hivi karibu kunyoa nwele zao hadharani kama hatua ya kuonyesha upinzani wao dhidi ya serikali ya Moon Jae -in
Hwang Kyo-ahn alinyolewa upara mbele ya wafuasi wake na wandishi wa habari nje ya kasri la raia Jumatatu jioni.
Upinzani wao ni dhidi ya waziri mpya wa sheria, Cho Kuk ambaye familia yake inahusika katika kashfa ya rushwa.
Wiki iliyopita, wanawake wawili wabunge walinyoa nywele zao kutokana na sakata hiyo hiyo.
Walionyoa vichwa vyao wanatoka katika chama cha kihafidhina na muungao unaoipinga serikali ya sasa ya rais Moon Jae-in.
Wanataka Bwana Cho ajiuzulu na afutwe kazi.
Maandamano haya yanahusu nini?
Cho Kuk, profesa wa zamani wa masuala ya sheria na mshirika wa rais Moon , alichukua mamlaka wiki iliyopita kama waziri wa sheria.
Lakini wakosoaji wake wana jazba kwamba aliteuliwa kuchukua wadhfa huo na Bwana Moon licha ya kuendelea wa shutuma za ufisadi kuhusu elimu na uhalifu wa fedha dhidi yake.
Mke wake, ambaye pia ni profesa , pia anasakwa kwa madai ya kugushi vyeti vilivyomsaidia binti yao kujiunga na chuo kikuu na kupata ufadhili wa masomo , jambo ambalo limeviudhi vyuo vikuu na wanafunzi wengine wa vyuo vikuu.
Waendesha mashtaka pia wanatafuta mwekezaji katika mfuko tata wa usawa unaodaiwa kuwakumuhusisha ndugu yake mwingine. Katika wiki za hivi karibuni , waendesha mashtakawalifanya uvamizi kadhaa katika familia ya Bi Cho.
Katika kikao cha kwanza cha kusikiliza madai dhidi yake Ijumaa , Cho alisema "anaomba msamaha sana kwa vijana waliokereka " juu ya madai ya kugushi vyeti kwa binti yake ''. Lakini akasema anataka kufanya mageuzi katika mfumo wa sheria.
Bwana Moon amesisistiza kuwa hakuna uthibitisho kuwa kulikuwa na hatua ya ukiukaji wa sheria na akasema itakuwa ni vibaya kutomteua mtu kwa misingi ya madai tu.
Lakini kesi hiyo imeibua mjadala kuhusu faida wanazopata walio nacho nchini Korea Kusini , ambayo imekumbwa na kashfa za ufisadi katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.
Serikali iliyopita ilipinduliwa kutokana na madai ya ufisadi na rais wa zamani Park Geun-hye kwa sasa anatumikia kifungo cha jela kwa kutoa hongo na matumizi mabaya ya mamlaka.
Bwana Hwang alihudumu kama waziri mkuu chini ya utawala wa rais Pak - na baadhi ya wachunguzi wa mambo wanasema umma unamuona kama mtu ambaye msimamo wake ni kuhujumu utawala wa sasa wa rais Moon Jae-in.
Ni kwanini wapinzani wakaamua kunyoa vichwa vyao?
Korea Kusini ina utamaduni wa kunyoa nywele kama aina ya upinzani.
Kitendo cha kyoa vichwa kinaonyesha mkanganyiko na kihistoria inaonyesha utashi wa kutaka kutatuliwa kwa
Katika miaka ya the 1960 na 1970 wakati Korea Kusini ilipokuwa chini ya utawala wa kijeshi wa udikteta , raia walikuwa mara kwa mara wakinyoa nywele zao kama ishara ya kupinga.
Katika miongo kadhaa iliyopita, wanaharakani na wanasiasa wamekuwa wakitumia njia hii kama njia ya kupinga jambo fulani.
Mwaka 2018, wanawake walinyoa vichwa vyao katika maandamano dhidi ya kuwekwa kwa kamera za ujasusi katika vyoo vyaona katika vyumba vya kubadili nguo kama njia ya kuwachunguza wanawake.
Miaka miwili kabla , zaidi ya wanawake 900 wa korea Kusini walinyoa vichwa vyao kama njia ya kuonyesha upinzani mfumo wa marekani wa kuzuwia makombora ya masafa.
Mnamo mwaka 2007,mamia ya wakazi wa mji wa Icheon walinyoa vichwa vyao kutokana na utata kuhusu eneo la ujenzi wa kiwanda.
Hwang alipeleka msimamo wa umma nje ya kasri ya rais, the Blue House, Jumatatu jioni.
Walimtaja Bwana Cho kama "mhalifu'' na kumtaka ajiuzulu.
Aliuambia umati wa watu uliokuwa ukimtazama akinyoa kichwa chake kuwa : " Niko hapa kutoa ahadi kuhusu malengo yangu kwa kunyoa kichwa changu . Sitarudi nyuma ."
Upinzani wake uliibua hisia katika mitandao ya kijamii . Tukio lake lilikuwa miongoni mwa taarifa 10 zilizosambaa zaidi katika mitandao ya kijamii katika orodha ya Naver, tarifa yake ikiwa ni moja ya taarifa zilizosakwa zaidi kupitia mtandao wa Google.
Many comments likened his looks to actor Gary Oldman - earning him the nickname Kimchi Oldman.