Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je hatma ya Grace Mugabe ndani ya Zimbabwe baada ya kifo cha mume wake ni ipi?
Kimekuwa ni kipindi kigumu nchini Zimbabwe.
Huku taifa likijaribu kushughulikia msiba huu uliotarajiwa kwa muda mrefu wa mpendwa , baba na muasisi wa taifa Robert Mugabe, limejipata likikabilina na mkanganyiko na kufichuliwa kwa hali ya utata, kumbu kumbu za mema yaliyopita , unafiki na hasira , vikijumuishwa na kile kinachoweza kufananishwa na tamthilia ya njama.
Katikati ya utata huu na mabadiliko inayopitia nchi, kuna Bi Grace Mugabe mwenye ukali - mjane ambaye anaomboleza, sura yake kwa sasa imejificha nyuma ya kitambaa cheusi cha shela mwanamke ambaye utajiri wake umeonyesha ni kwa kiwango gani mamlaka yana nguvu nchini Zimbabwe.
Alikuwa mpigachapa ambaye aliolewa na rais, ambaye wakati huo alipata umaarufu kwa mtindo wake wa kufanya shoping ya vitu vya beoi ghali na mwenye hasira . Grace alipata shahada ya udaktari yenye utata na akaingia katika siasa , kuongoza chama tawala cha Zanu PF akiongoza vuguvugu la wanawake wa chama hicho.
Ukosoaji wa Grace uliokithiri na utashi wake wa mamlaka ambao ulikuwa wazi viliaminiwa kuchochea mapinduzi yaliyotekelezwa na jeshi mwaka 2017 ili kumaliza vuguvugu lake ndani ya chama tawala na mipango yake ndani ya chama hicho.
Je kulikuwa kulikuwa na chuki miongoni mwa umma juu ya tabia yake? Bila shaka. Matokeo yanayoonekana dhahiri ya siasa zake yalikuwa ni kuitoroka nchi na kuondoshwa kikatili kutoka katika chama cha ZANU-PF
Lakini sasa amerudi. Na labda huenda ni kwa nia tu ya kumzika mme wake.
"Ana nguvu . Atabakia nchini Zimbabwe. Atadhalilishwa, lakini ataishi ," anasema Patrick Zhuwao, mpwa wa Mugabe na mmoja wa washiri wa kisiasa wa Grace ambaye aliamua kuishi nchi ya ng'ambo kwa ajili ya usalama wake.
Wiki iliyopita , Grace amekuwa mkimya , lakini amekuwa mwenye hasira mjini Harare, wakati mwingine hata anapokuwa mbele ya umma ambapo alikasirishwa juu ya mipango na siasaza ni wapo unakofaa kuzikwa mwili wa mume wake aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95.
Alionekana mtulivu wakati ndege iliyobeba sanduku la mwili wa mumewe kutoka Singapore lipotua mjini Harare. Alikataa mazishi ya kitaifa . Akavuruga mipango ya mazishi . familia ililalamika juu ya kulazimishiwa mazishi ya kitaifa.
Lakini nchini Zimbabwe - , ufisadi, mamlaka yaliyo mikononi mwa wachache na mtikisiko wa kisiasa unaweza kuwa ndio demokrasia - kila badiliko limekuwa likichunguzwa kwasababu huenda likafichua mengi juu ya mamlaka waliyonayo wasomi wanaoendesha mambo yao kisiri lakini wakati mwingine pia tukio linaweza kufanyika ili kuvuruga hasira kubwa ya umma juu ya madai ya utoaji wa sumu na mauaji.
Yamekuwa ni maswali ambayo wengi wanajiuliza. Je Grace anapanga kurudi katika siaza za Zimbabwe? Ninani anayeshinda vita vya kumrithi Mugabe? Je rais Emmerson Mnangagwa ameshinda au ametoa msamaha kwa hasimu wake? Je idadi ndogo ya watu waliojitokeza katika mazishiya kitaifa ilipangwa ili kuonyesha chuki kwa watu wa familia ya Mugabe ?
Ni kwanini hakuna mtu aliyepongeza hotuba iliyopambwa ya Mnangagwa ? Ni nani aliyebaki na mamlaka katika familia ya Mugabe - Grace au wazee wa ukoo. Ni kwanini Grace alidai yawepo makumbusho rasmi ya mume wake ? Je atakuwa salama Zimbabwe ? je anaweza kuwa na ushirikiano wa amani na Bwana Mnangagwa?.
Unaweza kuona ni kwanini wanauita tamthilia.
Ukweli ni kwamba Grace Mugabe atatakiwa kufanya mkataba wa aina fulani na serikali ikiwa atataka abakie na utajiri wake nchini Zimbabwe na usalama wake pamoja na wa familia security and family intact. Perhaps she already has.
Yeye na mumewe walidhani mamlaka yao ya kisiasa ni makubwa kupita kiasi na wakalaghaiwa na uungaji mkono mkubwa miaka miwili iliyopita alioishia kuwa na matokeo mabaya kwao wote wawili.
Alikuwa ni mwanaume mwenye huzuni, huzuni , huzuni sana ," alisema mpwa wake Mugabe , Walter Chidkhakwa, Jumamosi alipoelekea hali ya mjimba wake katika miezi yake ya mwisho ya uhai wake.
Hali ya baadae ya kisiasa ya Zimbabweinaonekana kuvurugika . Serikali inajaribu kutekeleza mageuzi magumu ya kiuchumi lakini inakosa imani ya umma na uwezo, umoja na haiba ya kuendeleza hatua muhimu za utekelezwaji wa mageuzi hayo.
matokei yake ni hali ya uchumi kuwa ngumu miongoni mwa wengi. Pengine lamsingi ni kwamba bado hakuna sdemokrasia upinzani unaamini kuwa uchaguzi wa mwaka jana ulitawaliwa na wizi wa kura, na unaweza kuamua kuingia mitaani kama walivyofanya wenzao nchini Kenya, kuchokoza kamata kamata ya maafisa wa usalama na mzozo na labda uweze kufikia mkataba wa mgawanyo wa madaraka.
wakati haya yote yakiendelea, huenda Grace Mugabeatabakia katika jumba lake la kifahari - Blue Roof - lililopo kaskazini mwa mji mkuu Harare - akisubiri kujengwa kwa jumba la makumbusho lenye thamani ya mumewe likamilike, na kujiandaa kwa mazishi ya faragha , na fursa moja zaidi ya kuwakemea waliomsaliti mme wake.