Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fahamu jinsi unavyoweza kuepuka kupata mzio kwenye mgahawa
Kwa watu wenye mzio wa vyakula, kula mgahawani ni changamto kubwa sana.
Na hii hutokana na kutofahamu viungo ambavyo vimetumika katika kuandaa vyakula hivyo.
Maelezo katika 'menu'(orodha ya vyakula ) yanaweza kuwa sio miongoni mwa vyakula ambavyo mteja au mlaji ana mzio navyo lakini vitu vilivyochanganywa kwenye chakula ndio vinavyoweza kumdhuru mtu.
Mfano mtu unaweza kuagiza nyama ya kuku lakini usijue ni viungo gani vimetumika vinaweza kukudhuru.
Lakini Je, migahawa inatakiwa kufanya? Na je wateja wa migahawa wanatakiwa kufanya nini ili kujilinda na mzio?
Nchini Uigereza migahawa mingi tayari inaonyesha vyakula vyenye vitu vya mzio, kwenye tovuti zao, vikiwemo vitu kumi na nne vinavyosababisha mzio kwa watu wengi zaidi, pembeni mwa kila chakula.
Kwa migahawa mingine huduma ya kuelezea kuhusu vyakula vya mzio inasaidia kadri watu milioni mbili nchini Uingereza wenye matatizo haya ya mzio.
Wateja wanaweza kuangalia 'menu' muda wowote ule na kuchagua vyakula kutokana na vitu gani zinavyoweza kuwadhuru.
Mtu anaweza kupoteza maisha hata kupata matatizo ya muda mrefu pale atakapokula chakula chochote ambacho kinaweza kumsababishia madhara.
Kwa bara letu la Afrika, ni migahawa michache sana inatoa huduma kama hizi.
- Onyo kwa wateja
Migahawa itoe onyo kwa wateja wote wanaoingia kwenye migahawa yao, bila kujali kama wana mzio na kitu chochote au hawana.
Migahawa ichapishe karatasi kama zile za Menu zikionesha maelezo kuhusu vyakula hatarishi kwa watu wenye mzio, na viungo vyote vinavyotumiwa vile ambavyo vinatumika kwenye vyakula vya mgahawa wao, na vilevile watengeneze karatasi ya menu inayoonyesha vyakula maalumu kwa watu wenye mzio.
- Waweke maelezo kwenye tovuti za migahawa yao.
Siku hizi watu wengi wanatumia mitandao mbalimbali kuperuzi vitu tofauti, Ikiwemo kuangalia migahawa gani ya kwenda kula chakula. Kwahiyo migahawa inatakiwa kuweka maelezo kuhusu vyakula gani vinaweza kuwa na viungo ambavyo vinaweza kuwa hatari kwa watu wenye aleji/mzio.
Vilevile wawaeleze wateja kuwa wanaweza kuuliza zaidi watakapofika kwenye mgahawa.
- Wateja wachague viungo vya kuweka kwenye chakula chao
Wateja wawe huru kuchagua viungo gani vitumike kwenye vyakula wanavyovitaka.
Mfano kama mtu ana aleji na maharage ya nazi, basi awe anaweza kusema yeye aletewe maharage ambayo hayana nazi.
Pamoja na kutengeneza sehemu ya kupikia vyakula maalum kwa watu wenye aleji. Viungo hatarishi visihifadhiwe kwenye sehemu hiii.