Utafiti: 'Wazazi sio lazima kumuadhibu mtoto '

Utafiti umebaini kuwa njia nzuri ya kumkanya mtoto asirudie kufanya jambo baya alilolifanya ni kumueleza mtoto kwa upole bila ya kumdhuru au kuharibu mahusiano yenu.

Licha ya mfumo huo wa kutowaadhibu watoto umekosolewa na wengi, lakini bado adhabu kwa watoto haijaweza kusaidia au kurekebisha tabia za watoto wengi, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa nchini Marekani.

Lakini mtafiti anasema kwamba , jambo la muhimu la kuzingatia wakati wa kutoa adhabu ni namna ambavyo adhabu hiyo inavyotolewa.

"Sio watoto wote huwa wanabadilika kwa kugombezwa au kupewa adhabu kali".

Utafiti huo kutoka chuo cha Michigan uliweza kuangazia familia zaidi ya 1400 na kuona jinsi wanavyolea watoto wenye umri wa miaka mitatu, mitano na kumi.

Watafiti waliweza kupima akili ya wote kuangalia mambo ambayo wazazi wanayapenda na hawayakubali, pamoja na kwa upande wa watoto kuangalia vitu wanavyopenda kuvifanya kama kucheza game, kugundua vitu na kurekodi video.

Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu, wazazi walimpa adhabu mtoto wao ya kumtaka kukaa kimya katika kona ya ukuta.

Pamoja na kwamba wazazi wanaendelea kutumia njia mbalimbali, utafiti umebaini kuwa adhabu hizo kwa watoto haziwezi kuleta utofauti wowote zaidi ya kuwapa msongo wa mawazo.

Wazazi ambao wanakanya watoto kwa adhabu au kufanya mambo tofauti na utaratibu, ukiwalinganisha na wazazi wengine ambao hawatumii mbinu hii kuna utofauti.

Katika uhalisi , wazazi ambao wanawaadhibu watoto kwa kuwapiga, watoto wanakuwa watukutu zaidi.

Miongoni mwa wazazi ambao walidai kuwa wanapata msongo wa mawazo ,

Watoto wao wana dalili kubwa za kutokuwa na furaha na kuishi kwa hofu pamoja na kuwa watukutu zaidi.

Lakini kwa mujibu wa utafiti, haijathibitishwa bado kuwa kumpa mtoto adhabu kunaweza kurekebisha tabia ya mtoto huyo.

Mara nyingi adhabu huwa hazieleweki'

Muandishi wa utafiti huo, Dkt Rachel Knight anasema kwamba mara nyingi wazazi huwa wanajiuliza kama huwa wanafanya jambo sahihi kwa watoto wao .

"Kinachoshangaza, wazazi wengi siku hizi wanaenda kutafuta ushauri katika mitandao ya kijamii au marafiki na sio wataalamu wa afya.

Kuna taarifa nyingi katika mitandao ambazo sio sahihi."

Aliongeza kusema kuwa kuna tafiti nyingi ambazo zimeandika namna ya kuwakemea watoto kwa upole kunavyoweza kutatua changamoto, kama mfumo huo utatumika vizuri .

"Mbinu za malezi mara nyingi huwa hazieleweki au zinatumika ndivyo sivyo."

  • Kutokuwa na jazba
  • kuwa na msimamo katika maamuzi
  • kuwa na mtazamo chanya
  • kuwa na mipango thabiti
  • kuwafanya wazazi na watoto kuelewa
  • Kutogomba

Dkt Helen Barrett phisiolojia mstaafu wa maendeleo anasema kwamba , kuwa na msimamo wakati unatoa ujumbe wako ni muhimu sana katika kumkanya mtoto.

"Ingawa kuna wazazi ambao wanaona ni lazima kuwaadhibu watoto wao lakini sasa watu wanapaswa kuelewa kuwa wazo la kuwaadhibu watoto limepita na wakati.

Huwa inategemea na watoto pia, adhabu mara nyingine huwa watoto wanaona kuwa ni unyanyasaji au kuaibishwa.

Huwa inategemea muda na sehemu adhabu hiyo inatolewa", alieleza.

Dkt. Barrett anasema kwamba uzuri kuna njia mbadala kwa mfano watoto kukanywa ndani ya vyumba vyao huku wakiwa wamekaa tu.

Lakini maeneo mengine, adhabu inatolewa adharani tena kwa kelele au viboko , jambo ambalo sio sahihi.

Njia nzuri ya malezi ni kuwa wakarimu na kutoonyesha jazba kwa watoto.."

Adhabu kubwa kwa watoto barani Afrika ni viboko.

Wazazi wengi barani Afrika, huwa wanapenda kutoa adhabu kwa watoto wao kwa kuwapiga viboko ikiwa ni sehemu ya kuwakanya.

Lakini madhara huwa ni kubwa kwa watoto;

Fimbo inauwa ubunifu,inasababisha watoto kuwa waongo na kuwafanya wawe waoga.

Mtoto anaweza kudanganya ili aweze kuepuka adhabu ya fimbo kitu ambacho sio sahihi katika makuzi ya watoto.

Viboko vinalazimisha watoto kukariri na kupunguza uwezo wa kufikiri.

Maonyo huweza kuwa maneno au vitendo elekezi na si viboko.

Asilimia 98 ya watoto wamedai kuwa wamekumbwa na adhabu ya kiboko

Hatuwezi kusema walimu hao wameua ilikuwa bahati mbaya kawa sababu kwenye kuua hakuna bahati mbaya.