Kwa nini maana ya ishara ya mkono imezua gumzo China?

Chanzo cha picha, TikTok/Sina Weibo
Video inayomuonesha msichana wa Kichina akitumia kiujanja ishara ya mkono kuomba msaada imesambazwa sana katika mtandao wa kijamii wa TikTok - hali inayoifanya mamlaka ya nchi hiyo kuingiwa na kiwewe.
Msichana huyo anaonekana akisindikizwa na mtu asiyemjua katika uwanja wa ndege.
Kwa sababu hakuwa alihofia wa kupiga mayowe ili apate usaidizi aliamua kuonesha ishara ya mkono iliyomaanisha mambo yako "SAWA".
Hatua hiyo iliwafanya wapita njia kubishana ikiwa msichana huyo alikua sawa au la lakini wengine waligundua kuwa anazuiliwa bila hiari yake. Baadae aliukutanishwa na wazazi wake.
Lakini kwa nini video hiyo iliyozua gumzo kali katika mitandao ya kijamii nchini China imeikasirisha mamlaka ya nchi hiyo?
Ishara ya mkono

Licha ya kuwa ishara inayomaanisha mambo ni "shwari" inajulikana na watu wengi duniani, nchini China maana ya ishara hiyo inaweza kubadilika ukigeuza mkono kidogo tu.
Vidole viwili vikishikana pamoja, na mkono wako uoneshshe ishara ya nambari"110" -Kwa Wachina inamaanisha kuwasiliana na polisi katika hali ya dharura.
Ktika video hiyo mhisika anaonesha ishara ambayo hata mtoto mdogo anaweza kung'amua kuwa unakabiliwa na tatizo.
Ili kuhamasisha jamii kuhusu ishara hiyo mwisho wa video hiyo kuna mwanamume anaewaambia watu "sambaza ujumbe huu" ili watu waitumia wanapotaka usaidizi" kama pengine wametekwa nyara na wanahofia maisha yao".
Mamlaka haipendelei ishara hiyo

Chanzo cha picha, Piyao
Video hiyo inaonekana kama tangazo la kibiashara kwa umma, kwa hivyo watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii walidhania linaungwa mkono na polisi.
Gazeti la kibiashara la kila siku linalofahamika kama Chengdu Economic linasema kanda hiyo ya video inayosambazwa katika mtandao wa TikTok inaonesha kana kwamba imetolewa na polisi.
Hata hivyo aliyenasa video yenyewe hajabainika mpaka sasa
Tayari vyombo rasmi vya habari vinawasilisha ujumbe wa mtandao wa kukabiliana na taarifa ghushi unaofahamika kama Piyao, kukosoa video hiyo kwa upotoshaji na kuongeza kuwa polisi hawana uhususiano wowowte na kanda hiyo ya video.
"Ishara kama hiyo haina msingi wowote ikitumiwa kuomba musaidizi wa dharura," ulisema, ishara hiyo haisaidii ikiwa anayeitumia hajui maana yake halisi hawezi kupata usaidizi anaotafuta.
Linaongezea kuwa halijawahi "kutangaza ishara hiyo kwa umma ili watu watumie wakiwa katika hali ya hatari", na kutoa wito kwa watu kufuata mfumo wa jadi wa kupiga simu polisi wakiwa katika hali ya hatari ili wapate usaidizi.

Chanzo cha picha, Taobao
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wanafikiria ni wazo zuri
Licha ya mamlaka kujitenga na kanda hiyo ya video na kampeini yake kupata umaarufu wa ghafla katika mtandao wa TikTok, imezua mjadala mkali ikiwa ishara hiyo inaweza kutumiwa kuwafanya Wachina wajue ikiwa mtu anakabiliwa na hali ya hatari.
Baadhi yao katika mtandao maarufu wa Sina Weibo wanasema "kupiga mayowe kama ishara ya kuomba msaada kunasidia zaidi badala ya kuonesha ishara", huku wengine wakisema ishara huenda ikatafsiriwa visivyo hali ambayo inaweza "kuwapotosha watu" na kusababisha hali ya taharuki.
Lakini katika nchi zilizo nda utawala wa kiimla watu hawana uhuru wa kujieleza hadharani, baadhi yao wanasifia lugha ya ishara katika mazingira kama hayo ambayo wanafananisha na mtu aliyetekwa nyara.
"Lugha za ishara inaweza kusaidia nchi", mmoja wa watumiaji wa lugha hiyo alisema.
"Alimradi kila mtu anaielewa, tunaweza kuitumia ," mwingine alisema. "Bora sote tunaelewa maana ya ishara inayotolewa hakuna shida."
Nambari kama ishara ya uasi
Baadhi ya nambari kwa muda mrefu zimetumiwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii kukosoa serikali bila ya maana halisi kujulikana.
Watu wamegundua mbinu ya kuzungumzia mauaji ya Tiananmen Square ya mwaka 1989 - ambayo serikali iliweka siri kwa miongo mitatu- kwa kutumia nambari fiche kama "46"kumaanisha (4 Juni), "64" (Juni 4) au "1989".
Mamlaka ilibaini maana ya nambari hizo na imekuwa ikiweka vikwazo kuhusu utumizi wake lakini hiyo haimaanishi kuwa ujumbe unaojumuisha nambari hizo zinafutwa.
Mwimbaji Taylor Swift - ambaye alikuwa maarufu sana China - alipozindua albamu 1989, serikali ilikua na wakati mgumu kufuatilia ujumbe unaoangaziwa katika muziki wake.
Kulikua na hofu huenda muziki wake unatumia maana fiche kupitisha ujumbe wenye utata katika historia ya hivi karibuni ya China.

Chanzo cha picha, AFP













