ATCL: Ndege ya Tanzania imetua nchini baada ya kuachiliwa huru Afrika kusini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Damas Ndumbaro (katikati)pamoja na maafisa wengine kabla ya ndge kuondoka kuelekea Tanzania

Chanzo cha picha, Wizara ya mambo ya nchi za nje ya TanzaniaTwitter

Maelezo ya picha, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Damas Ndumbaro (katikati)pamoja na maafisa wengine kabla ya ndge kuondoka kuelekea Tanzania
Muda wa kusoma: Dakika 2

Ndege ya Air Tanzania imetua nyumbani Tanzania mwendo wa saa mbili unusu usiku huu baada ya kuachiliwa huru na mahakama ya Afrika Kusini.

Shirika la ndege hiyo imeandika katika ukurasa wake wa Tweeter kuwa safari za ndege hiyo kuelekea Afrika kusini zitarejea siku ya ijumaa.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Mapema leo Mahakama Kuu ya jimbo la Gauteng imeamuru ndege ya Air Tanzania iliyokuwa ikishikiliwa nchini Afrika Kusini kuachiwa mara moja.

Mwandishi wetu wa Afrika Kusini Nomsa Maseko anasema kuwa utaratibu wa kuiachia ndege hiyo kurejea Dar es Salaam kutoka uwanja wa ndege wa OR Tambo jijini Johannesburg unaendelea.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Damas Ndumbaro aliyekuwepo mahakamani ameileza BBC kuwa Tanzania imeridhishwa na uamuzi wa mahakama

Chanzo cha picha, Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Tanzania/witter

Maelezo ya picha, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Damas Ndumbaro aliyekuwepo mahakamani ameileza BBC kuwa Tanzania imeridhishwa na uamuzi wa mahakama

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Damas Ndumbaro aliyekuwepo mahakamani ameileza BBC kuwa Tanzania imeridhishwa na uamuzi wa mahakama.

Mkulima ambaye alipeleka shauri hilo mahakamani Hermanus Steyn na kupata kibali cha kushikiliwa ndege hiyo, hakuridhishwa na hukumu ya awali na kukata rufaa.

Mwandishi wa BBC Maseko anaripoti kuwa Bw Steyn amedondoshwa pia kwenye rufaa yake na kutupiliwa mbali na mahakama.

Jaji Twala

Chanzo cha picha, Nomsa Maseko/BBC

Maelezo ya picha, Jaji Twala M L akisoma hukumu yake mapema leo na kuamuru ndege ya Tanzania kuachiwa

Dkt Ndumbaro ambaye pia ni wakili amesema kama Steyn bado ana madai yeyote, inafaa arudi kwenye mahakama za Tanzania na kusikilizwa.

"Oh, niamini, raisi (John Magufuli) tayari ameshapewa taarifa (ya hukumu)," mwandishi wa BBC aliyepo mahakamani anamnukuu Dkt Ndumbaro akisema.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Ndumbaro pia amesisitiza kwa kuwa serikali ya Tanzania imeshamlipa Steyn dola milioni 20, maana yake wapo tayari kumalizia bakaa ya deni, lakini mkulima huyo "anatakiwa kurudi katika mahakama za Tanzania, na aache kuihusisha Afrika Kusini."

Baada ya ya kushindwa kwa kesi ya awali na hatimaye rufaa, wakili wa Steyn ameiambia BBC kuwa uamuzi wa mahakama: "Ni kushindwa moja kwa moja kwa haki, na mteja wangu anaona kuwa ameonewa. Bw. Steyn amepoteza kikomboleo cha mali na hii inamaanisha kuwa hawezi kukata rufaa bila ya ndege kuwa imezuiliwa."

Jaji aliyesikiliza rufaa amesisitiza kuwa Afrika Kusini haina mamlaka ya kisheria (jurisdiction) ya kuliamulia jambo hilo.

Kwa nini ndege ilizuiliwa?

Ndege hiyo aina ya Airbus A220-300 ilikuwa imeshikiliwa katika uwanja wa Oliver Tambo jijini Johannesburg kwa amri ya mahakama.

Hermanus Steyn alifungua kesi ya fidia dhidi ya serikali ya Tanzania.

Steyn alikuwa anamiliki ardhi, mifugo na mali nyingi ambazo zilitaifishwa na serikali ya Tanzania miaka ya 1980.

Ilipofika miaka ya 1990 walikubaliana fidia atakayolipwa, kwa ujumla wake dola milioni 33 na tayari ameshalipwa dola milioni 20 kati ya hizo.

Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Tanzania, kwa mujibu wa mkulima huyo imeacha kulipa deni hilo, na hatua ya kuomba ndege kushikiliwa ilikuwa moja ya harakati zake za kutaka kumaliziwa deni.