China yashtushwa baada vifaa vya msaada waliotoa kutoweka Kenya

Chanzo cha picha, SIMON MAINA
China imesema imeshtushwa na taarifa iliyopokea kutoka kwa bunge la Kenya kuwa kontena lililokuwa na vifaa vilivyotolewa kama msaada kutoka China na kuwasili siku ya Jumanne na kufunguliwa na maafisa wa bunge la Kenya lilikuwa tupu.
Taarifa nchni zinaashiria kuwa kontena hilo lenye vifaa vya msaada lilipelekwa katika makao ya bunge liliwasili likiwa halina kitu ndani.
China imesema tukio hili ni la kwanza kuwahi kutokea ,na kwamba kwa miaka mingi imekuwa ikitoa misaada ya kirafiki kwa Kenya, ikiwemo vifaa tiba, vifaa vya ofisi, msaada wa chakula nakadhalika, na vyote vimekuwa vikiwasilishwa vikiwa salama kabisa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
BBC imezungumza na msemaji wa jeshi la polisi nchini Kenya, Charles Owino ambaye aliulizwa kuhusu taarifa za kuwasili kwa kontena kutoka kwenye viwanja vya bunge likiwa tupu, alieleza kuwa hana taarifa kabisa kuhusu taarifa hizo isipokuwa kupitia mitandao.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
''Kwa kawaida huwa tunapata briefing kutoka kwa mkuu wa polisi na sijui kama ni mambo ya mitandao ya kijamii ama ni kweli kwa sababu sijapata taarifa kwa mkuu wa upelelezi hivyo pengine niulizie halafu baadae tuweze kuzungumza''.
Amesema pia hana habari kama kontena hilo liliwasili likiwa tupu.
Katika hatua nyingine, uchunguzi unaripotiwa kuidhinishwa kupitia idara ya makosa ya jinai nchini katika kinachotajwa na vyombo vya habari Kenya kuwa ni kubaini mazingira yaliyojitokeza ya kontena hilo kutoka China kuwasili Kenya likiwa tupu.
Tukio hili limewagusa raia wengi wa Kenya huku baadhi wakisema kuwa ni jambo lililoiabisha Kenya.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Vifaa vilivyoorodheshwa vikiwa pamoja na kompyuta mpakato, na projekta zilikuwa msaada kutoka Bunge la taifa la China na mzigo huo ulipaswa kufikishwa Kenya kupitia ubalozi wa China nchini Kenya.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 4

Mwisho wa X ujumbe, 5
Katika taarifa iliyowasilishwa siku ya Jumatano, Karani wa Bunge la Kenya, Michael Sialai amethibitisha kuwa kontena lililowekwa nembo ya 'mizigo ya kidiplomasia' liliwasili siku ya Jumanne, tarehe 30 mwezi Julai mwaka 2019 kama ilivyotarajiwa lakini baada ya kufunguliwa, hakukuwa na kitu ndani yake, Televisheni ya Citizen ya Kenya imeripoti.
Kwa mujibu wa karani wa bunge la Kenya, ubalozi wa China jijini Nairobi iliingia mkataba na kampuni ya usafirishaji iliyojulikana kwa jina M/S Bollore Africa Transport & Logistics Ltd kusafirisha kontena hilo.
''Kweli kontena liliwasili katika viwanja vya bunge tarehe 30 mwezi Julai, 2019, ambapo niliwateua maafisa kadhaa kutoka kwenye bunge waweze kuthibitisha mzigo kwa ulinganifu na kile kilichoelezwa kuwasilishwa na ubalozi wa China,'' ilieleza taarifa ya Sialai.
''Baada ya kufungua kontena, ilithibitishwa kuwa lilikuwa tupu. Wakala na maafisa wetu kwa pamoja walinifikishia suala hilo na kuamua kuwa maafisa wa DCI wapatiwe taarifa hiyo, suala ambalo lilifanyika ipasavyo''.
Baada ya uthibitisho kuwa kontena lililowasilishwa na kampuni ya M/S Bollore Africa Transport & Logistics Ltd lilikuwa tupu, maafisa wa DCI waliripotiwa kutoa taarifa kwa ubalozi wa China wakati uchunguzi ukiendelea.
Kutolewa kwa msaada wa vifaa vya elektroniki kwa ajili ya bunge uliwekwa wazi wakati wa ziara ya makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge la watu wa China na ujumbe wa maafisa wa China tarehe 13, mwezi Aprili mwaka 2019.
Hakuna uthibitisho kuhusu mahali au lini vifaa hivyo vya kielektroniki ambavyo thamani yake haijafahamika vilitolewa na kutoweka.