Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uingereza: Wapasuaji waunganisha mkono uliokatwa kwa msumeno
Fundi seremala ambaye mkono wake ulibaki ukining'inia kati ya ngozi na mfupa baada ya kupata ajali mbaya ya kukatwa na msumeno wa umeme amefanikiwa kufanyiwa upasuaji wa kuungwa mkono huo.
Anthony Lelliott, mwenye umri wa miaka 46, mkono wake wa kushoto ulikuwa karibu kukatika wote katika sehemu mbili wakati alipokuwa anakata bodi ya sakafu kwa mashine yenye nguvu .
Alifanyiwa upasuaji kwa muda wa saa 17 katika hospitali ya Mt.George huko kusini mwa London.
Madaktari hao wanasema kuwa kesi yake ilikuwa kubwa ambayo hawajawahi kukutana nayo kabla.
Mtaalam wa upasuaji wa plastiki, Roger Adlard alifanya operesheni ya awali kwa saa 13 akishirikiana na mwenzake Farida Ali.
Adlard alisema: "Kuna wataalamu wengi wa upasuaji ambao, wangeona ukubwa wa jeraha, wangefikiria kuwa asingepona,
Lelliott alikuwa amekatikatika na meno ya msumeno huo na halikuwa jeraha lililonyooka."
Mkono wa Lelliott ulikuwa bado umeshikana lakini kwa ngozi tu na mfupa mdogo.
Alipoteza damu nyingi na hakuwa na kumbukumbu ya ajali iliyompata.
Lelliott anasema kwamba hata haelewi mkono wake ulifikaje kwenye msumeno.
Anahisi labda ubongo wangu ulikuwa haufanyi kazi sawa, lakini hali ile ilikuwa nje ya jinsi alivyokuwa anajisikia katika mwili wake.
"Nilikuwa nnajiona mwenyewe na namna ambavyo nilipaswa kufanya. Damu ilikuwa imetapakaa kila sehemu.
Kile ambacho ninakikumbuka ni jinsi nilivyokuwa natoka nje na kusalimiwa na watu wengi ambao hata nilikuwa siwezi kuwasahau."
Adlard alisema akiwa nje ya chumba cha upasuaji kuwa majeraha yake yalikuwa makubwa zaidi ya walivyofikiria.
"Ilikuwa sio kuunga mkono tu, bali mishipa na mirija ya kusukuma damu pia ilipaswa kuirejeshe katika hali yake ya awali .
Majeraha hayo yameelezewa kuwa ni suala la kuunga mkono jambo ambalo sio la kweli.
Ingawa mkono huo ulikuwa umekata kabisa katika vipande viwili - chini kidogo ya vidole - na kupelekea jeraha kuwa kubwa mara bili.
"Nilijua kuwa upasuaji huu utachukua muda mrefu," mtaalamu wa upasuaji alieleza.
Katika upasuaji wa kwanza ,timu ya upasuaji walifanya usiku mzima kuhakikisha kuwa kuna msukumo mzuri wa damu na mishipa inapeleka damu katika vidole vingi iwezekanavyo.
Baada ya kuunga mfupa uliokuwa umeharibika, walitoa mishipa ya miguu.
Umakini mkubwa ulikuwa unahitajika kwa ajili ya kuunga kila kitu.
Madaktari wanasema kuwa waligundua kuwa sehemu ya ngozi ya Lelliott ilikuwa imepata maambukizi ya vimelea na kidole chake cha katikati kiliharibika vibaya sana hivyo kisingeweza kupona.
"Tumefanya maamuzi ya kuona namna ya kuokoa mkono wote, inabidi kidole cha katikati kiondoke ili kisaidie kuweka ngozi kuwa sawa na mfupa ulitoka katika mkono.
Tatizo lingine lilikuwa ni kupata ngozi ya kutosha kufunika eneo hilo.
Mkono wake hauwezi kurudi katika hali yake ya kawaida , tuna matumaini kuwa kuna namna ya ufanyaji kazi wake utarudi kuwa kama awali lakini anaweza kukunja mkono na kushika hata kalamu kuandika."
Kwa upande wake bwana Lelliott amefurahia huduma nzuri aliyoipata, "Ninashukuru kila mmoja aliyenihudumia, maneno hayawezi eleza kwa sababu nilikuwa nitakuwa nnaamka bila kuwa na mkono wngu mmoja. Kwa sasa ninajaribu tu kuzoea namna ya kuutumia, ninashukuru sana".