Raia wa India alisukuma hadi ndani ya mto gari alilozawadiwa siku yake ya kuzaliwa

Raia mmoja wa India aliyekasirishwa kwa kupewa zawadi ya gari aina la BMW kusherehekea siku yake ya kuzaliwa -badala ya gari aina ya Jaguar alilisukuma gari hilo na kuliingiza mtoni.

Kanda ya video iliochapishwa katika mitandao ya kijamii iliionyesha gari hilo likiolea katika mto huo katika jimbo la kaskazini mwa India la Haryana.

Gari hilo baadaye lilisukumwa hadi katika kingo za mto huo na mwanamume huyo anayedaiwa kuwa mwana wa mmiliki wa nyumba kadhaa katika eneo hilo akajaribu kuliokoa.

Maafisa wa polisi wanachunguza kisa hicho, kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo.

Gari la BMW linagharimu zaidi ya 3.5m rupees { $49,000} nchini India huku lile la Jaguar likigharimu 4-5m rupees.