Hakuna la kujitetea kwa neno ''tumbili'', asema binti yake Ronald Reagan

Chanzo cha picha, Getty Images
Mtoto wa kike wa rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan amesema " hakuna la kujitetea "kwa kauli alitotoa mwaka 1971 katika mazungumzo ya simu.
Mkanda mpya wa sauti umefichua Reagan -ambaye wakati huo alikuwa Gavana wa California - aliuelezea ujumbe wa Afrika katika Umoja wa Mataifa kama "tumbili".
Binti yake Patti Davis amelaani vikali katika waraka wake uliochapishwa katika gazeti.
"Hakuna la kujitetea ,hakuna ufafanuzi wa maelezo, hakuna ufafanuzi mzuri juu ya kile ambacho baba yangu alikisema ," aliandika.
Bi Davis aliandika katika waraka kwa ajili ya gazeti la Washington Post kwamba alikuwa anajianda kumtetea baba yake kabla ya kusikia kanda ya sauti, lakini alishituka baada ya kusikia kile alichokisema rais huyo wa zamani.
"Siwezi kuwaambia kumuhusu mwanaume aliyekuwa akiongea kwa simu ," aliandika . "si mwanaume niliyemfahamu mimi."
Ni nini alichokisema Ronald Reagan?
Sauti iliyorekodiwa hivi karibuni ilionekana kwa mara ya kwanza katika gazeti la The Atlantic.
Reagan alitoa kauli katika mazungumzo na rais wa Marekani aliyekuwa madarakani wakati huo -President Richard Nixon.

Chanzo cha picha, Getty Images
Alikuwa akiuelezea ujumbe wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa(UN), ambao walikuwa upande wa wapinzani wa Marekani katika kura dhidi ya kuitambua Uchina na kuiondoa Taiwan katika Umoja wa Mataifa.
Reagan - ambaye ni anaiunga mono Taiwan - alimpigia simu rais siku iliyofuata ,akimwambia : "Aaangalie hao ... tumbili kutoka hizo nchi Afrika - ambao bado hawafurahii kuvaa viatu!"
Nixon anasikika kwenye ukanda huo akiangua kicheko kwa sauti kubwa baa ya kauli hiyo.
Binti yake Reagan aliandika nini?

Chanzo cha picha, AFP/GETTY
Patti Davis alisema ukanda ulimshitua . "ninataka kurejea nyuma wakati bado sijasikia sauti ya baba yangu akisema maneno."
Baba yake , aliandika, alipambamba dhidi ya ubaguzi alipocheza soka alipokuwa chuonina baadae alipoingia madarakani alipopewa uanachama wa "klabu ya taifa ya ritzy mjini Los Angeles".
"aliikataa kwasababu klabu haikuwaruhusi Wayahudi au Wamarekani wenye asili ya Afrika."
Aliandika kuwa maneno aliyoyasikia "Yatabaki nami daima ", na akasema kama baba yake angekuwa badi hai "angeomba msamaha " kama angesikia sauti yake iliyorekodiwa.
Kauli zake "Haziwezi kueleweka kwa maneno mengine isipokuwa ubaya ", Bi Davis aliandika. Aliongeza kuwa anatumai watuwatamsamehe rais huyo wa zamani wa marekani "kwa manene ambayo hayangepaswa kutamkwa katika mazungumzo yoyote yale ," na ambayo "kwetu tuliomfahamu Ronald Reagan, yatabakia kuwa si ya kawaida."
Wakosoaji wanamshutumu Reagan kuwa mbaguzi wa rangi katika kipindi chake chote cha maisha ya kazi.
Alipokuwa akigombea kiti cha ugavana wa California mnamo mwaka 1966, mchezaji huyo wa zamani wa filamu alisema "kama mtu binafsi anataka kuwabagua waniga (Negroes) au wengine katika kuuza au kubodisha nyumba, ni haki yake kufanya hivyo ".
Kama rais, alijaribu kuzuwia muswada ambao ungeweka vikwazo dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Bunge lilipiga lilikwenda kinyume na veto yake na kuuidhinisha.
Reagan alikanusha shutuma za ubaguzi wa rangi dhidi yake.














