Utafiti: Mwezi Julai ulivunja rekodi ya joto duniani

heatwave

Chanzo cha picha, Getty Images

Uchunguzi wa awali unaashiria kuwa viwango vya joto duniani vilipanda sana mwezi Julai na kuvunja rekodi duniani.

Uchunguzi wa viwango vya joto vya siku 29 za kwanza za mwezi huo katika baadhi ya nchi unaonesha kuwa joto lilipanda na kuvunja rekodi iliyokuwepo mwezi Julai mwaka 2016.

Utafiti uliofanywa na shirika Muungano wa Ulaya linaloangazia masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa maarufu Copernicus Climate Change Service(C3S).

Kuthibitishwa kwa rekodi hii mpya ya viwango vya joto kutasubiri hadi matokeo kamili ya utafiti yatakapotangazwa Jumatatu wiki ijayo.

chart

Je kuongezeka kwa joto kiasi hiki ndio ushahidi wa mabadiliko ya tabia nchi?

Prof. Peter Stott- Mkuu wa idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini uingereza anasema: Kama ni hali ya hewa ya kawaida ambayo haijachafuliwa na binadamu, tunaweza kuona joto la mara moja moja lakini tunapoona joto la kupita kiasi basi linatokana na mabadiliko ya tabia nchi na huenda binadamu ndio amechangia''

Wanasayansi wengine wanasema ni ishara wazi kwamba dunia inakabiliwa na dharura ya tabia nchi.

Ripoti mpya iliyokusanywa na C3S inajumuisha matokeo ya uchunguzi wa mitambo ya satellite na vituo vya ardhini.

Presentational grey line
how much warmer is your city -promotional image
Presentational grey line

Viwango vya joto vya mwezi Julai vinakadiriwa kuwa vya juu zaidi kuwahi kurekodiwa na shirika hilo katika kipindi cha miaka 40.

Kwa mujibu wa Copernicus, kila mwezi mwaka huu umeurodheshwa miongoni mwa miezi minne ya joto jingi ikilinganishwa mwezi uliochunguzwa na amabao umevunja rekodi.

Japo watafiti hawajahusisha moja kwa moja ongezeko hilo la viwango vya joto na mabadiliko ya hali ya hewa, baadhi ya wanasayansi wanahisi hali hiyo imechangiwa na ongezeko la hewa chafu aina ya carbon kutokana na shughuli za binadamu binadamu.

Mo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maelfu ya wazima moto wakikabiliana na moto wa mwituni nchini Ureno mwezi Julai

Ongezeko la joto duniani ulifanya mwezi wa Juni kuwa wa joto kali zaidi kuwahi kuonekana jambo lililowafanya wadadisi na wanaharakati wa mazingira kuonya kuhusu dharura ya tabia nchi.

"Mwezi huo ulikuwa na joto jingi lakini si hayo tu ni kwamba miezi yote ya mwaka 2019 imeshuhudia viwango vya juu vya joto," Dr Freja Vamborg kutoka Copernicus aliiambia BBC.

"Na mwenendo huo huenda usibadilike ikiwa suala la gesi chafu halitashughulikiwa ."

Joto limekuwa likiongezeka duniani kote tangu karne ya iliyopita lakini miaka minne iliyopita joto lilikuwa kali zaidi.