Mazingira: Bendi ya Fulu yatunza mazingira kwa kubadilisha takataka kuwa vifaa vya muziki

Je! Umewahi kufikiria kusikiliza bendi iliyo na vyombo vinavyotengenezwa kutoka na takataka? Mjini Kinshasa kuna bendi ya muziki ambayo huitwa fulu muziki au muziki wa takataka.
Bendi hiyo hainunui vyombo vya muziki lakini inatengeneza yenyewe vyombo vyake
Wao hutumia vitu mbali mbali walivyookota kutoka kwenye taka, sio tu kwa nia ya kuburudisha, watumbuizaji hao wamekua wakichangia katika kutunza mazingira.
Mwandishi wa BBC Kinshasa Mbelechi Msoshi alikutana nao.
Kwanza huchakura taka na kuchukua vipande vya,chupa,mabomba yaliyoharibika,na vitu vingine ambavyo vinaweza kuzalisha sauti nzuri ya muziki,bendi hio ya mziki inafahamika kama fulu, ikiamanisha mziki wa taka taka. Baada ya kuvicheza vipande vilivyopatikana kwenye taka, sauti nzuri hupatikana.
Pisco Crane ni jina lake la usanii na jina lake rasmi ni Ewango Mabende, yeye ni Kiongozi wa bendi hiyo iliyoanza mwaka 2016.
Lengo kuu ni kupambana na uchafuzi ya mazingira, kupitia mziki wake ,vile vile alitaka kuhamasisha serikali na raia kuhusu kuondokana na takataka nyingi ambazo zimejaa ndani ya mji mkuu wa Kinshasa na zinazoweza kusababisha mangojwa.
"Watu ambao wanatupa taka kando ya makazi ya raia wanashindwa kuondoauchafu huo, na katika pita pita zangu,nikaona ya kwamba kuna namna yakuchangia ili kujaribu kupunguza uchafu mjini,wakati naona kitu Fulaniambacho naweza kuchukua na kukipa thamani tena; mfano mzuri ni sisiwatu ambao tunaishi karibu na taka hizo tunapata magonjwa yanyotokanana mrundikano wa takataka.Taka ni kitu kibaya sana katika mazingira''.
Aisha ni msichana pekee kati bendi hio .Anasema ''Tuna leta mziki mpya wa mitaa, sisi ni waasanii, hatuwezi baki katikamuziki ambao unazungumzia tu masuala ya ngonoinabidikuleta mabadiliko,kuelimisha watu pia kuhusumazingira,hususani watoto wajue kulinda mazingira. Mimi nilijiunga nabendi hiiwakati niliposikia mziki wao unaweza kubadilisha ulimwengu na wala siotu Kinshasa.''
Kuna vitu havikuwa ndani ya muziki wao, lakini fulu music imeleta mambo mapya.
Watu walifikiri mzaha, hawakuamni kuwa bendi hii imepata umaarufu mkubwa leo.
Matumaini ya piscro crane ni kuona mziki wake unakubalika duniani kote.












