Familia za waathiriwa wa ajali ya Lion Air ''zadanganywa juu ya fidia''

Abiria wote 189 waliokuwemo ndani ya Lion Air walikufa mwezi Octoba mwaka jana

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Abiria wote 189 waliokuwemo ndani ya Lion Air walikufa mwezi Octoba mwaka jana

Ndugu wa watu waliouawa katika ajali ya ndege aina ya Boeing 737 Max iliyopata ajali nchini Indonesia mwaka jana wamekuwa wakidanganywa ili wasipatiwe fidia, wamesema mawakili wao.

Mawakili wao wameiambia BBC kuwa familia nyingi zilishawishiwa kusaini fomu zinazowazuwia kuchukua hatua za kisheria.

Kipindi cha BBC cha Panorama kimegundua kuwa jamaa wengine wa waathiriwa walisaini makubaliano sawa na hayo baada ya ajali nyingine mbili, zilizowazuwia kuishtaki kampuni ya Boeing katika mahakama za Marekani.

Boeing imekataa kutoa kauli yoyote juu ya makubaliano hayo.

Abiria wote 189 na wahudumu wa ndge walikufa wakati ndge ya Boeng 737 Max ilipoanguka baharini dakika 13 tu baada ya kuondoka kutoka katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta tarehe 29 Octoba 2018.

katika kipindi cha wiki kadhaa, ndugu wa waathiriwa walilipewa fidia na mawakili wa kampuni ya bima.

Merdian Agustin
Maelezo ya picha, Merdian Agustin anasema alishinikizwa kusaini nyaraka

Ili kupata pesa, familia zililazimika kusaini makubaliano ambayo yangezizuwia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Boeing au ndege ya , Lion Air.

Mme wa Merdian Agustin , Eka, alikufa katika ajali hiyo. Anasema mawakili wa bima walijaribu kumshinikiza asaini kinyume na haki yake.

"Walinipatia waraka kusaini. Waraka huo ulisema unaweza kupata pesa lakini huwezi kuishtaki Lion Air. Huwezi kuishtaki Boeing.

"Walisema unapaswa kusaini hii. lazima usonge mbele . Katika kipindi cha saa moja au saa mbili utapata pesa na utaendelea na maisha, lakini sitaki pesa . Inahusu mme wangu ", alisema.

Bi Agustin hakusaini,lakini inaaminiwa kuwa familia zipatazo 50 zilisaini. Watapata fidia ya chini ya $92,000 kila mmoja.

Malipo yana utata kwasababu chini ya sheria ya Indonesia familia zina haki ya kupata fidia ya pauni 71,000.

Sanjiv Singh, ambaye ni wakili anayewawakilisha baadhi ya watu wa familia zilizowapoteza ndugu kwenye ajali hiyo , ameiambia BBC kuwa ndugu wamekuwa wakishinikizwa kusaini kinyume cha haki zao.

"Familia zilizosaini nyaraka hizo zimedanganwa katika fidia , zimelaghaiwa na makampuni ya bima na kwa ushauri wa mashirika hayo ya bima kwa ajili ya faida ya Boeing" alisema.

Aliongeza kuwa familia hizo zilikuwa na haki ya kupata mamilioni ya dola ya fidia.

Hii sio mara ya kwanza kwa Boeing kunufaika kutokana na nyaraka za fidia za waathiriwa wa ajali ya ndege.

Mnamo mwaka 2005, Boeing 737 ilianguka kwenye eneo la makazi ya watu nchini Indonesia, na kuwauwa watu 149. Familia zilisaini makubaliano ambayo yalizuzuwia kuishtaki which prevented Boeing katika mahakama za Marekani . JMakubaliano kama hayo yalisainiwa baada ya ajali ya 737 iliyowauwa wasafiri 102 mnamo mwaka 2007.

Wakili mmoja ambaye jina lake halikutajwa alihusika katika maytukio yote matatu.

Bwana Singh anasema hii inaibua maswali mengi juu ya ikiwa Boeing ilihusika katika mapatano ya hivi karibuni ya Lion Air.

Panorama iliiuliza Boeing kama ilifahamu juu ya mapatano au ilikuwa na mawasiliano yoyote na mawakili wa bima waliosaidia kuandaa malipo ya ndugu wa waathiriwa.

Boeing haikujibu swali lolote ililouliwa na kipindi cha Panorama na badala yake ilitoa taarifa iliyosema: "Boeing kusema ukweli inasikitishwa na kupotea kwa maisha na itaendelea kushirikia na jamii, watejana sekta ya usafiri wa anga katika mchakato wa matibabu ya kisaikolojia.

"Bima za Boeing ziko katika mazungumzo na bima nyingine duniani, kama ilivyo kawaida wanapokuwa katika hali kama hizi."

Bima kuu ya Lion Air na Boeing ni ya Uingereza ya kampuni ya Global Aerospace.

Sanjiv Singh
Maelezo ya picha, Sanjiv Singh, wakili wa familia, anasema zinahitaji pesanyingi zaidi ya zile walizopewa

Global Aerospace ilipinga madai, lakini ikakataa kutoa kauli yoyote juu ya madai hayo kwasababu ya kulinda siri ya mteja.

Ilisema: "Ni kawaida kwa kampuni ya bima ya safari za ndege kuweka bima kwa zaidi ya kbima moja kwa mtu ambayer amehusika kwa namna fulani katika ajali.

"Global Aerospace, kulingana na utendaji wa sekta, hugawa wajibu kwa ajili ya kuwashughulikia wateja tofauti ili kuhakikisha kila mteja anawakilishwa kivyake, na kwa hilo hakuna ushirikishaji usiofaa wa taarifa unaofanyika katika kushughulikia dai lolote linaloweza kutokea."

Kampuni hiyo imesema kuwa ni utendaji wa kawaida wakati wanapotatua madai kuwasaidia watengenezaji wa ndege kutohusika na mashtaka kwa siku zijazo.

tarehe On 3 Julai Boeing ilitangaza kuwa itatoa dola milioni 100 kusaidia jamii na familia zilizoathiriwa na ajali ya ndege yake 737 Max . Ya pili ilikuwa ni ya Ethiopia Aprili, ambapo watu 157 walikufa

Mawakili wa familia wanasemahawajapewa maelezo juu ya jinsi pesa hiyo itakavyotumia.