Kampuni Boeing yatangaza kuboresha ndege yake ya 737 Max

Muundo na mfumo wa uongozaji wa ndege ya Boing 737 Max uliripotiwa kuwa chanzo cha ajali zake

Chanzo cha picha, Getty Images

Boeing imeboresha mfumo wake ndege ya chapa -737 Max- iliyopigwa marufuku kufuatia ajali zilizosababisha vifo vya abiria wengi katika kipindi cha miezi mitano.

Kampuni hiyo ya Marekani imetangaza kuwa tayari imekwishafanya safari 270 za ndege ya 737 Max yenye programu iliyoboreshwa.

Imeongeza kuwa itatoa taarifa kwa utawala wa safari za anga nchini Marekani-Federal Aviation Administration (FAA) -juu ya namna rubani anavyowasiliana na waongozaji wa ndege na hatua anazopaswa kuchukua kwa matukio mbali mbali.

FAA inatarajia Boeing iwasilishe taarifa juu ya namna ilivyoboresha ndege yake kwa ajili ya kupewa idhini ya kupaa tena wiki ijayo.

Ndege ya Ethiopian Airlines ilianguka mwezi Machi na kuwauwa watu wote 157 waliokuwemo.

Ndege aina ya Boeing 737 Max-8 iliyomilikiwa na Ethiopian Airlines iliyoanguka mwezi Machi 2019 na kuwauwa watu wote 157

Chanzo cha picha, JONATHAN DRUION

Ajali hiyo ilifuatia mkasa wa Lion Air nchini Indonesia mwezi Octoba ambapo watu 189 walikufa.

Ajali zote mbili ziliihusika kasoro ya mfumo wa Boeing 737 Max -ambao ulikuwa ni mpya uliolenga kuboresha udhibiti wa ndege na kuizuiwia kuelekeza uso wake juu.

Kifusi cha ndege ya Ethiopian Airlines katika eneo la ajali iliyotokea mwezi Machi, 2019

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Boeing ilisema kuwa mara taarifa juu ya namna marubani wanavyoonyeshwa jinsi ya kutumia mfumo ulioboreshwa itakapowasilishwa kwa FAA, itashirikiana na wafuatiliaji wa usalama wa ndege kufanya majaribio ya safari za ndege na kuwasilisha hati ya mwisho.

Mapema wiki hii FAA ilisema kuwa itafanya mkutano na waangalizi wa usalama wa safari za anga tarahe 23 Mei kutoka kote duniani kuwapatia taarifa za sasa juu ya tathmini ya mfumo ulioboreshwa wa Boeing na mafunzo mapya kwa marubani.

Unaweza pia kutizama:

Maelezo ya sauti, Familia zaomboleza mkasa wa ajali ya ndege Ethiopia