Tetesi za soka Ulaya Jumapili 16.06.2019:Salah, Pogba, Diop, Jesus, Maguire, Benteke, Kessie

Mohamed Salah

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah, 27, amekataa ofa ya uhamisho ya pauni 150 milioni kutoka vilabu vya Real Madrid na Juventus. (Mirror)

Kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba, 26, yupo tayari kuanza mgomo ili kushinikiza uhamisho wake kwenda Real Madrid. (ABC - in Spanish)

United pia wanampango wa kumsajili beki Mfaransa Issa Diop, 22, kwa dau la pauni milioni 45 kutoka West Ham. (Sky Sports)

United ambayo inanolewa na Ole Gunnar Solskjaer pia inaonekana kupokwa tonge mdomoni na Barcelona ambao wapo tayari kutoa dau la pauni 150 milioni ili kumng'oa Antoine Griezmann, 28, kutoka klabu ya Atletico Madrid. (Mirror)

Ole Gunnar Solskjaer

Mshambuliaji Marcus Rashford, 21, huenda akaongezewa mshahara mpaka kufikia pauni 350,000 kwa wiki na klabu yake ya Man United ikiwa ni moja ya njia za kumshawishi akatae ofa za usajili kutoka vilabu vya Real Madrid na Barcelona. (Sun)

Mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, 22, amesema "si jambo la kuuliza" iwapo yeye na mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 31, wataihama Manchester City kabla ya msimu ujao kuanza. (Mail)

Kiungo wa Chelsea Mfaransa Tiemoue Bakayoko, 24, amesema anatamani siku moja kuchezea klabu ya Paris St-Germain. (L'Equipe - in French)

Kocha Rafa Benitez amebakiza wiki mbili tu kumaliza mkataba wake na klabu ya Newcastle na bado hakuna makubaliano ya nyongeza ya mkataba. (Newcastle Chronicle)

Beki wa Leicester na England Harry Maguire, 26, alikubaliana na mmiliki wa klabu hiyo ambaye sasa ni marehemu Vichai Srivaddhanaprabha kuwa angeruhusiwa kuhama baada ya kukamilika kwa msimu uliopita. (Mirror)

Harry Maguire

Chanzo cha picha, Rex Features

Klabu ya Juventus ipo tayari kumsajili beki wa kulia wa Tottenham na England Kieran Trippier, 25, kwa dau la pauni 45 milioni. (Times - subscription required)

Mshambuliaji wa Ubelgiji, Christian Benteke, 28, anataka kusalia katika klabu ya Crystal Palace licha ya kuhusishwa na taarifa za kuhamia Ligi ya Uchina. (Standard)

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameambiwa na uongozi wa klabu hiyo kuwa ahakikishe anapata mbadala wa wachezaji wawili wanaondoka klabuni hapo, mlinzi Alberto Moreno, 26, na mshambuliaji Daniel Sturridge, 29. (Star)

Klopp, 52, pia yupo kwenye mikakati ya kusajili kipa namba mbili wa kikosi hicho wakati huu ambapo kipa Simon Mignolet, 31, anatarajiwa kuondoka. Klopp anatazamia kumnasa kipa wa Southampton Alex McCarthy, 29, ambaye atakuwa akimsaidia chaguo namba moja Alisson. (Mirror)