Lady Latrine: 'Kwa nini huwa anaweka picha za vyoo mtandaoni'

Chanzo cha picha, Lady Latrine
Mwanamke ambaye amejikuta kuwa huwa anatumia vyoo vya umma kila mara ameeleza jinsi alivyoanza kuvipiga picha na kuweka mtandaoni ili kuwafurahisha marafiki zake.
Lady Latrine, anajulikana kwa kuwa na wafuatiliaji wengi wa instagram kwa picha zake za vyoo katika nchi yake Cambridgeshire .
Mwanamke huyo huwa anatoa viwango vya ubora ,vyoo 10 kwa vigezo vya usafi , anasema kuwa huwa aoni aibu kufanya hivyo bali anafurahia.
"Nimefanya hivyo mara nyingi ili kutofautisha kati ya vyoo visafi na vichafu," alisema.
Mwanamke huyo alianza kuweka picha za vyoo vya umma mwezi machi akiwa hajaweka utambulisho wa jina lake.
"Niliamua kufanya hivyo kwa sababu nilikuwa na mtoto mdogo na kila nikienda kutumia choo cha umma nilikuwa napata mawazo kutokana na ubaya wa vyoo hivyo ," Latrine alieleza sababu ya kupiga picha vyoo na kuweka mtandaoni.

Chanzo cha picha, Lady Latrine

Chanzo cha picha, Lady Latrine
Yeye ana picha za maliwato kuanzia hoteli za gharama mpaka migahawa ya kahawa.
Huwa anaangalia ubora kwa picha na urembo uliotumika katika choo pamoja na ubora wa sabuni zinazotolewa .

Chanzo cha picha, Lady Latrine

Chanzo cha picha, Lady Latrine
Bi.Latrine anasema kuwa anajaribu kuweka usawa kwa picha anazoweka kwa sababu kuna sehemu huwa kuna shughuli nyingi lakini bado wanaweka mazingra safi ya vyoo.
Hii ni kutokana na jitihada kubwa ambayo watu hao wameamua kujitoa ili kuhakikisha usafi wa vyoo unazingatiwa.
"Ni kawaida kukuta vyoo vya hoteli za gharama vikiwa na muonekano wa kuvutia lakini kwa kumbi za starehe kukuta iko safi vyooni ni lazima kiwango cha ubora kiwe juu kwa sababu si jambo la kawaida lazima nguvu kubwa imetumika" Latrine asimulia.
"Sina lengo la kudhalilisha maeneo au mhusika basi kuwapongeza wale ambao wamefanya kazi nzuri ya kuhakikisha kuwa vyoo ni visafi.
Ndio maana nilianza na choo changu mwenyewe kuonesha namna kilivyo kisafi"Bi.Latrine alisisitiza.












