Wanaume waonywa dhidi ya upasuaji wa urembo

Man having forehead injected

Chanzo cha picha, Getty Images

Shinikizo la kutaka kuwa na muonekano mzuri ni kubwa kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake wengi wakiishia kufanyiwa upasuaji wa urembo ili kulifikia hilo.

Hayo ni kwa mujibu wa shirika moja la wataalamu Uingereza wanaofanikisha urembo huo kwa wanaume.

Wameonya kwamba hatari ni nyingi kutokana na mbinu hizo za urembo na hii ni wakati BBC Imefanya uchunguzi nchini humo ulioashiria kwamba takriban 50% ya wanaume walio na umri wa kati ya miaka 18-30 "huenda wamefikiria" kufanyiwa mageuzi mwilini kupata muonekano mzuri.

Na idadi ya wanaume wanaotafuta urembo kupitia njia hizi za upasuaji inaongezeka na wataalamu wanasema ni jambo la kawaida maana ni mkonodo unaoshudiwa kote duniani.

Nchini Kenya kwa mfano hamu ya kuwa na umbo dogo la mwili, rangi nyeupe ya ngozi au tabasamu la kuvutia ni jambo la kawaida kutokana na idadi ya wateja wanaotembelea kliniki za urembo huo mfano madkatai wa meno kusafisha au kuchubua rangi ya meno yatakate zaidi.

hair transplant Kenya
Maelezo ya picha, Mteja katika kliniki moja Kenya akipandikizwa nywele

Na dhamira ni sawa kwa wote, sio tu Kenya lakini hata katika maenoe mengine Afrika, wanaume hutafuta urembo huo kupata muonekano mzuri na kuvutia zaidi.

Kuna wanaopendelea kubadilisha umbo lao, kuvutia wapenzi wapya, au kumtia gere mpenzi ulioachana naye.

Wengine ni kuiga mifano ya maisha ya nyota wa matiafa ya magharibi, kuiga mitindo na huenda likachukuliwa kuwa jambo lisilo na maana lakini kwa wateja kuna sababu kuu ya mtu kuamua kupitia kisu cha mpasuaji.

Na urembo huu huwafanya baadhi hata kusafiri kwenda nchi za nje kama Ulaya na hata bara Asia kufanyiwa upasuaji.

Kuna mtindo ambao mfano mzuri umedhihirika ulaya kwa mchezaji soka Wayne Rooney wa kukiondposha kipara kichwani, Wanaume katika nchi za Kiafrika mfano Kenya wanatafuta suluhu ya tatizo la kukatika nywele zao kwa kufanyiwa upandikizaji.

Save Face linasema wanaume wengi Uingereza huingia katika mtandao wao kuliko hata wanawake na wamepokea ripoti za malalamiko zilizoongezeka za waliofanyiwa upasuaji wa urembo uliokwenda vibaya na sasa wanahitaji usaidizi.

"Kuna ongezeko la wanaume wanoafanyiwa upasuaji wa aina hii na pia wanaum wanaokabiliw ana matatiazo wakati upasuaji unapokwenda vibaya," anasema Ashton Collins kutoka kundi hilo.

Anasema picha katika mitandao ya kijamii na vipindi katika televisheni ndio chanzo cha wanaume wengi kutaka kubadili umbo lao.

Katika utafiti wa BBC uliohusisha wanaume 2,000 na wanawake, waliulizwa ni sehemu ipi ya mwili waliopenda kuibadili - 34% ya wanaume wengi walisema tumbo lao na kifua.

Diren Kartel mkufunzi binafsi wa mazoezi ya mwili anasema hashangazwi na chaguo hilo kwa wanaume.

"Hata mimi nilipoanza kufanya mazoezi nilitaka kuwana msuli tumboni uliokazana. Nilipokuwa kijana nilitaka kuwana tumbo gumu lenye msuli, ndilo jambo ambalo kila mwanamume angependa kuwa nalo.."

Doctor marking patient with pen

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini anaonya kwamba ukarabati huo haumaanishi mtu ana afua nzuri na badala yake anapendekeza kufanya mazoezi na kula chakula kizuri chenye afya ili mtu apate mwili anaoutaka.

Ashton Collins kutoka Save Face ana wasiwasi kwamba baadhi ya wanaume huenda wakaishia kufanyiwa upasuaji mbovu kwasaabu ya kuona aibu ya kuzungumzia hamu walio nayo.

Anaeleza kwamba bado kuna vizingiti katika kulizungumzia hili wazi kama ilivyo kwa wanawake na urembo jambo ambalo linazidi kuhatarisha wanaume kufanyiwa upasuaji visivyo.

Na zaidi kwa wanao kwenda katika mitandao ya kijamii na kuchunguza kliniki za bei nafuu zinazofanya upasujai wa aina hii, ambao mwisho wa kwisha wanahatarisha uzima au afya zao.

line