Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Songkran: Thailand inaadhimisha tamasha la kibudha kwa vita vya maji
Wathailand wanasherehekea mwaka huu kwa tamasha la Songkran , unaofahamika pia kama mwaka wa Wabudha
Tamasha hilo ambalo hufanyika kati ya tarehe 13 na 15 Aprili nchini Thailand, pia husherehekewa katika maeneo mengine kama Laos, Cambodia and Myanmar.
Songkran hujulikana mara kwa mara kama kama vita vikubwa vya maji duniani.
Picha kutoka kote nchini Thailand zinaonyesha umati mkubwa wa watu wakishiriki sherehe hizo.
Siku hiyo ya mapumziko zamani ilikuwa ikiadhimishwa kwa wanafamilia kuimwagia maji sanamu ya Budha.
Katika picha hii, watu wanainyunyizia maji sanamu ya Budha.
Zamani kurusha maji kulimaanisha kuosha mikosi ya mwaka uliopita.
katika picha hii (juu) ndovu na watu wanaonekana wafukiza maji.
maelfu kwa maelfu ya watalii huenda thailand kila mwaka , hususan katika mji wa Bangkok na miji mingine kushuhudia tamasha la Songkran.
Watu wengi hushiriki wakiwa wamevalia nguo zenye rangi mbali mbali za kuvutia katikasherehe hizi. Katika picha hii (chini) mvulana mdogo ameketi kwenye mabega ya mtu huku akicheza na maji akifyatua maji.
Tarehe 15 Aprili, siku ya kwanza ya mwaka wa Thailand , watu hukusanyika katika mahekalu kutoa chakula na nguo mpya kwa watawa kama sadaka.
katika picha hii (chini) watu wakimpiga maji mtu ambaye amelala chale sakafuni.
Picha zote zina hakimiliki