Rubani wa Emiliano Sala, David Ibbotson alikiuka sheria

Chanzo cha picha, Getty Images/David Ibbotson
Rubani wa ndege iliyoanguka wakati ikiwa na mchezaji Emiliano Sala, anaelezwa hakuwa na vigezo vya kurusha ndege wakati wa usiku, BBC imeelezwa.
David Ibbotson anaelezwa kuwa na tatizo la kutotofautisha rangi (colour-blind), na leseni yake inamruhusu kurusha ndege wakati wa mchana pekee.
Mcheza soka Sala,28 alipoteza maisha ndege hiyo ilipombeba kutoka Nantes kuelekea Cardiff tarehe 21 mwezi Januari.
Mamlaka ya anga nchini Uingereza (CAA) imesema haitazungumza chochote.
Ofisi inayofanya uchunguzi kuhusu ajali za anga imesema kuwa leseni ni kitu kinachotiliwa mkazo kwenye uchunguzi wake.
Mamlaka zimethibitsha kuwa Bwana Ibboston hakua na vigezo vya kurusha ndege usiku
Leseni yake inaeleza kuwa ''anapaswa kuwa na miwani imsaidie kuona karibu''

Chanzo cha picha, AAIB/Google Earth
Chanzo kutoka mamlaka ya anga kimesema uwezo wa kutofautisha rangi ya kijani na nyekundu ni ''muhimu'' wakati wa kuruka usiku.
''Chochote kilicho kwenye leseni ya Uingereza kinatekelezwa hivyo hivyo nchini Marekani, hivyo asingeweza kufanya chochote zaidi ya kile leseni inamruhusu kufanya.
Kufanya kazi nje ya matakwa ya leseni ni kinyume cha sheria.
Sheria ya mamlaka ya anga ya bara la ulaya inatafsiri usiku kuwa ''muda kutoka nusu saa baada ya jua kuzama mpaka nusu saa kabla jua kutoka''.
Mipango ya safari inaonyehsa ndege ilipangwa kumbeba mchezaji wa Argentina Sala kwenda kwenye mazoezi ya kwanza na timu ya Cardiff City ilitakiwa kuondoka Nates saa tatu kwa saa za uingereza tarehe 21 mwezi Januari.
Lakini ndege iliahirishwa mpaka saa moja jioni baada ya ombi la Sala, ili aweze kuwaaga wachezaji wenzake wa Nantes.
Mpaka Bwana Ibbotson anaipeleka ndege kwenye njia tayari kwa kuruka muda mfupi baada ya saa moja, ingekuwa muda wa saa moja na dakika 10 tangu kuzama kwa jua.

Chanzo cha picha, BBC Sport

Chanzo cha picha, PA/AAIB
Katika mahojiano mwezi Februari, wakala ambaye alikodisha ndege,aliiambia BBC kuwa yeye na familia yake walilipia ndege hiyo.
Hakuhusishwa, alisema katika kuchagua ndege wala kuchagua rubani.
Ndege ilitoweka kwenye rada kaskazini mwa Guernsey saa mbili na dakika 16.
Mwili wa Sala ulipatikana kwenye mabaki ya ndege mwanzoni mwa mwezi Februari lakini mwili wa Ibbotson haujapatikana.

Chanzo cha picha, AFP
Mamlaka ya usalama wa anga ulaya inasema kuwa na kigezo cha kurusha ndege usiku, rubani lazima apitie mafunzo ya kurusha ndege usiku kwa saa tano sambamba na mafunzo ya saa tano ya nadharia.
Katika ripoti ya awali, mamlaka hiyo imesema kitabu na leseni vilipotez.hivyo wameshindwa kufahamu ni kwa saa ngapi ameweza kurusha ndege hivi karibuni ingawa imefahamika kuwa ameruka kwa saa takriban 3,700.
Wanaofanya uchunguzi huangalia ni kwa saa ngapi rubani amerusha ndege katika kipindi cha siku 28 na 90 kabla ya ajali.
Mamlaka hiyo inatarajiwa kutoa ripoti kamili kuhusu ajali hiyo mwanzoni mwa mwaka 2020.












