Rais wa Algeria awania nafasi ya urais kwa mara ya mwisho akiwa na miaka 82

Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, amepuuza wito wa kumtaka kutowania tena urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi ujao.

Bouteflika ametoa msimamo huo katika siku ya mwisho ya kuwania fomu za kuwania urais.

Kwa siku kadhaa sasa kumekuwa na maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali ya taifa hilo yanayolenga kupinga hatua ya rais huyo kuwania tena nafasi hiyo.

Baada ya kuwasilisha fomu maalum ya uchaguzi, kwa niaba ya kiongozi huyo, meneja wake wa kampeni, Abdelghani Zaalane, amesoma barua iliyoandikwa na Rais Bouteflika,

akieleza kwamba amesikia kilio cha waandamanaji na atakapochaguliwa atafanya mabadiliko.

"Kama Mungu akipenda na kama waaljeria watarejesha Imani yao kwangu, nitatekeleza wajibu wa kihistoria ili kufanikisha mahitaji yao ya msingi: ambayo ni kubadili mfumo".

Aidha ameahidi kuitisha upya chaguzi ndani ya mwaka mmoja, ambapo hatowania tena kiti hicho.

"Nina ahidi kuandaa uchaguzi wa mapema kupitia mjadala wa huru wa kitaifa. Na naahidi sitagombea ktk uchaguzi huo".

Rais Bouteflika, mwenye umri wa miaka 82 sasa , ameonekana mara chache hadharani tangu aanze kuugua ugonjwa wa kiharusi mwaka 2013.

Nani wanagombea nafasi ya urais?

Mpaka sasa kuna wagombea wengine sita ambao wamejiandikisha kuwania nafasi hiyo, miongoni mwao akiwemo Ali Ghediri, ambaye alihaidi kuleta mabadiliko nchini Algeria.

Mfanyabiashara Rachid Nekkaz, ambaye ana wafuasi wengi kwenye mtandao wa kijamii na anatajwa kuwavutia vijana wengi nchini humo, alitangaza nia yake lakini hakukidhi vigezo.

Ingawa binamu yake Rachid Nekkaz ambaye ni fundi magari aliweza kuingia katika kinyang'anyiro hicho na mfanyabiashara huyo maarufu amedai kuwa ataongoza kampeni za ndugu yake.

Mpinzani mkubwa wa chaguzi ziliopita Ali Benflis, atagombea nafasi hiyo tena.

Je, maandamano haya ni kitu kipya ?

Maandamano ya aina hii nchini Nigeria ni jambo ambalo ni adimu kutokea Algeria na maandamano yameonekana kuwa makubwa tangu Bouteflika aingie madarakani miaka 20 iliyopita.

Maandamano yalianza siku 10 zilizopita mara baada ya Bouteflika kutangaza mipango yake ya kuwania nafasi ya urais kwa mara nyingine.

Polisi wameripotiwa kuwamwagia maji ya machozi wanafunzi waliokuwa wakifanya maandamano katika mitaa ya mji mkuu wa Algiers .

Vilevile kuna maandamano nchini Ufaransa dhidi ya ya utawala wa kikoloni , eneo ambalo raia wengi wa Alrgeria wanaishi huko.

"Hatumpingi raisi lakini kiuhalisia tu hana nguvu tena ya kuongoza,ni kama hayupo kabisa na wale watu ambao wako karibu yake ndio wanafanya kazi" mmoja wa waandamanaji aeleza.

Abdelaziz Bouteflika ni nani?

Bouteflika aliingia madarakani mwaka 1999 na kusifiwa kwa kutokomeza vita ya wenyewe kwa wenyewe ambayo ilikadiriwa kuuwa watu zaidi ya 100,000.

Waandamanaji dhidi ya ongezeko la gharama ya chakula na ukosefu wa ajira mwaka 2011 wakati wa utawala wa kiarabu , rais huyo aliweza kutatua tatizo hilo kwa haraka.

Mara baada ya kupooza , aliweza kushinda tena uchaguzi licha ya kuwa na upinzani mkali kutoka kwa vyama vya upinzani kwa kudaiwa kuwa afya yake itamfanya ashindwe kutimiza majukumu yake.

Pamoja na ukosoaji huo bwana Bouteflika bado ana nafasi kubwa ya kushinda mwaka huu.

Upinzani nchini Algeria umegawanyika na Bouteflika alishinda uchaguzi wa awali wa urais wa mwaka 2014 pamoja na kutofanya kampeni mwenyewe.