Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Rais wa Algeria amtimua Waziri mkuu
Bouteflika
Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria amemfukuza kazi waziri wake mkuu Abdelmadjid Tebboune, ambaye aliteuliwa katika nafasi hiyo miezi isiyozidi mitatu.
Hakuna sababu zilizotajwa za kuondolewa kwake kazini.
Lakini hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya Rais kumtumia barua kali bwana Tebboune kutaka mabadiliko ya sera.
Tayari waziri mkuu mpya ametajwa kuwa ni Ahmed Ouyahia ambaye alikuwa mnadhimu mkuu wa Rais.