Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 02.03.2019 Bale, Eden, Monreal,Dixon

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid itaangalia utaratibu wa kumuuza mshambuliaji Gareth Bale,29,kipindi cha majira ya joto (AS in Spanish)
Inahofiwa huenda mshambuliaji wa Tottenham Hary Kane akaondoa klabuni hapo kama timu hiyo itaendelea kuwa na ukame wa kutwaa mataji(Telegraph)
Chelsea wako kwenye mazungumzo na mshambuliaji Eden Hazard. (Le10Sport in French)
Manchester United iko kwenye mpango wa kumsajili beki wa kushoto Alex Sandro, 28, ikiwa ataamua kuondoka Juventus. (Tuttosport - in Italian)
Nacho Monreal wa Arsenal na beki wa kushoto wa Liverpool Alberto Moreno, 26 wananyemelewa na Barcelona.(Sport - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji raia wa Korea Kusini Son Heung-min,26, amebainisha nusura aondoke Tottenham baada ya msimu wa kwanza kwa kuwa hakufurahia msimu huo .(Standard)
Isaac Hayden wa Newcastle ameweka wazi kutaka kuiacha klabu hiyo ili awe karibu na mchumba wake na bintiye.Mchezaji huyo mwenye miaka 23 amesema familia yake imepitia kipindi kigumu ilipokua ikipata mtoto(Times - via Newcastle Chronicle)
Arsenal wanajianda kumsajili kinda wa miaka 17 wa Brazil Gabriel Martinelli kwa dau la pauni Milioni 4. (Goal via Mirror)
Wakati huo huo The Gunner ni moja ya klabu inayowania saini ya beki wa kushoto wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico(ESPN)
Beki wa Chelsea Mnigeria Ola Aina mwenye Miaka 22 inatarajiwa kukamilisha uhamisho wa kiasi cha pauni milioni 8.7 kujiunga na Torino ya Italia baada ya kufanya vizuri wakati wa mkopo akiwa na klabu hiyo ya Seria A.(Goal)
Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgos amesema mchezaji wake Beki Aaron Wan-Bissaka anaendelea kutilia mkazo katika timu yake licha ya tetesi kutakiwa na Man United. (Express)
Beki wa zamani wa Arsenal Lee Dixon amesema. Kiungo Denis Suarez hatochagua kusalia Arsenal kama ataendelea kutumika kama mchezaji wa akiba mchezaji huyu yuko kwa Mkopo klabuni hapo akitokea Barca (Evening Standard)
Beki wa Southampton Wesley Hoedt amesema anataka kusalia nchini Hispania katika klabu ya Celta Vigo wakati muda wake wa mkopo utakapomalizika mwishoni mwa msimu (Read Southampton)












