Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Senene: Mradi wa kula wadudu wavutia Benki ya Dunia na WHO
Wanasayansi katika mojawapo wa vyuo vikuu nchini Kenya wako kwenye harakati za kurai watu wale wadudu.
Ni miaka kumi na miwili tangu chuo kikuu cha kilimo na Teknolojia cha Kenyatta kuanza mradi wa wadudu.
Mradi huo umeyavutia mashirika ya kimataifa kama vile Benki ya Dunia, Shirika la Chakula Ulimwenguni ambayo yanaamini kuwa kilimo cha wadudu ni dawa nzuri ya kukabliana na uhaba wa chakula.
Shirika la Chakula Ulimwenguni, linabashiri ongezeko la mahitaji ya chakula, huku vipande vya ardhi vikiendelea kudidimia ifikapo mwaka 2050.
Inakadiriwa kwamba ifikiapo mwaka huo idadi ya watu ulimwenguni itakuwa imeongezeka hadi watu bilioni 10.
Protini
Wanasayansi sasa wanatarajia kuwa wadudu hawa wadogo wenye virutubisho watachangia kuziba mwanya wa uhaba wa chakula.
Wanasema kuwa wadudu hao wana protini zaidi ya mara tatu ukilinganisha na nyama ya ng'ombe, mara mbili zaidi ya samaki na kuku.
Prof Kinyuru anasema kuwa chuo hicho kinamiliki yamkini wadudu milioni mbili.
''hebu tafakari, nafasi ya ng'ombe milioni mbili, kuku milioni mbili, ni eneo bunge lote.Hakika protini hii nzuri ina madini ambayo mwili wako unahitaji. Kuna madini ambayo huwezi ukapata kwenye samaki ama kuku.
Kwa kipindi cha miezi mitatu senene huwa wako tayari kuliwa. Wao huanza kufa wakiwa na mieiz minne.
Lakini baada ya chuo kikuu kukabiliana na kiunzi cha kuhuisha wadudu hawa, chuo hicho kingali na kibarua kikubwa hata zaidi.
Na kutokana na hali hiyo, wengi afadhali wafe njaa kuliko kuwala wadudu.
Wengi wanazidi kubadili fikra zao
Hata hivyo profesa Kinyuru na kikundi chake wanasema kuwa wameona watu wengi ambao wamebadili mawazo yao na kufunza zaidi ya wakulima 2000.
Usiku wa kati ya mwezi Novemba na Disemba nchini Uganda huwa ni baraka, kwani huja na chakula chenye rotuba na kitamu.
Senene, huingia eneo la Lyantonde, mji ulioko umbali wa takriban kilomita 200 kutoka mji mkuu wa Kampala
Ambrose Sendagi ni mmoja wa wamiliki wa mitego ya senene, inapofika usiku wa manane, yeye huanza harakati za kwenda katika mitego mingine, zaidi ya maili 100 kabla ya jua kuchomoza.
Ambrose Sendagi: Ninaomba Mungu kuwa hali itaendelea kuwa hivi kabla ya upepo kuwahamisha. Huwa wanahamishwa na upepo na mwangaza.
Anaelezea kwamba wakati mmoja senene hao walikuwa wakizuiliwa na mwangaza mkali, na hivyobasi kutumbukia ndani ya mitego wakati ujuzi huo ulipoanza kutumika.
Hatahivyo anasema kuwa wakati mwengine upepo huwa mkali zaidi na hivyobasi kuharibu mitego.
Soko la Senene Uganda
Katika soko la Nakasero, mjini Kampala, wafanyibiashara wanaanda senene, huku wateja wakijawa na hamu.
Wengine huwapenda senene hao wanapokuwa na mbawa. Wanaweza kukaangwa ama kuandaliwa bila mafuta.
Nchini humo senene huliwa sio kama chakula, lakini wanasayansi wanasema kuwa ni chakula kikamilifu chenye protini.