Utalii Uganda: Shutuma kali dhidi ya kutumia umbo la wanawake kama kivutio Uganda

Waziri wa utalii nchini Uganda amependekeza kuwe na onyesho la wanawake wenye maumbo makubwa ili kuvutia wageni zaidi wanaoitembelea nchi hiyo.

Godfrey Kiwanda alielezea mpango huo wakati wa uzinduzi wa ukurasa wa pamoja, Miss Curvy Uganda,katika mji mkuu Kampala.

Akinyoosha mkono wake kwa washiriki wa zoezi hiko alisema kuwa, alisema kuwa wanawake wote wanaojumuisha walikuwa "hadithi tunayouza" kwa wageni.

Maoni ya Mr Kiwanda yametajwa kama "udhalili" na "kudhalilisha", na kumeanzishwa harakati nchini Uganda ili kupata mpango ingawa mpango huo umepingwa.

Akizungumza katika uzinduzi wa kivutio hicho mapema wiki hii , waziri huyo alisema kuwa itakuwa "tukio la kipekee ambalo litawaonesha mabanati wakionesha maumbo yao mazuri yaliyo nona"

"Tumepewa uwezo wa kawaida, wanawake wenye kutazamika ambao wana mvuto machoni kuangalia," tovuti ya habari ya Uganda ya Daily Monitor ilimnukuu akisema. "Kwa nini hatutumii watu hawa kama mkakati wa kukuza sekta yetu ya utalii nchini Uganda?"

Kauli hiyo haikupokelewa vyema nchini humo hasa kwenye mitandao ya kijamii kulichafuka ujumbe wa aina kwa aina Bila shaka, kulikuwa na sintofahamu katika mchakato wa kukuza sekta ya utalii nchini humo na wanaharakati wa kutetea haki za wanawake, ama wanawake wenyewe walionona nao walifurukutwa kutoa maoni yao.

Watu wengine walimshutumu bwana Kiwanda kwa kuzungumza juu ya wanawake wanono kama kwamba walikuwa kama wanyama walioko katika bustani ya wanyama, na mwanamke mmoja alihoji kama ingewezekana basi wawekwe bustanini ili watazamwe kama wanayama watendewavyo ".