Kwa picha: Watu 2 wanaofanana na Rodrigo Duterte na Kim Jong-un wazua vioja Hong Kong

Huenda ukadhania kwamba rais wa Ufilipino Rodrigo Durtete na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un walikuwa pamoja katika barabara za mji wa Hong Kong, wakipiga picha na kula pamoja chakula cha jioni katika mgahawa mmoja.

Lakini uchunguzi wa kina ulibaini kwamba wawili hao walikuwa watu waliowaiga viongozi hao wawili.

Kutana na jamaa anayejiita Cresencio Extreme anayefanana na Durtete na Howard X anayefanana na Kim Jong un.