Raisi Durtete ambusu mwanadayaspora jukwaani

Rais wa Philippine Rodrigo Duterte, amezua gumzo baada ya kumbusu mfanyakazi aishiye ughaibuni kwenye midomo hadhrani .Bwana Durtete alikuwa akizungumza na maelfu ya wa Korea Kusini na ndipo alipomwita mwanamke huyo apande jukwaani na kumshawishi kumbusu midomoni.

Tukio hilo lenye utata lilitukia wakati raisi Duterte akizungumza na umati wa wafanyakazi wa nchi za nje wa UFilipino (OFWs) huko Seoul.na kusababisha hisia mchanganyiko za umati wa watu, hasa wafanyakazi ambao ni raia wa Ufilipino waishia Korea Kusini.Kwanza alianza taratibu kumkumbatia mwanamke wa kwanza na kisha kumpa busu kwenye shavu kabla ya kumwita mwanamke wa pili na kumtaka ambusu midomoni .

Baada ya kutakiwa kumbusu raisi mwanamke huyo alirudi rudi nyuma kwa kusita juu ya ombi hilo, na kisha kuachilia kicheko cha mshangao kutoka pia na ishara za mara kwa mara za mwito kutoka kwa raisi Duterte, , rais hatimaye alishinda na kumbusu mwanamke huyo kwenye midomo na kuzua malalamiko mtandaoni.Lakini ilielezewa na kundi la kutetea haki wa UFilipino liitwalo Gabriela.

kuwa yalikuwa ni "maonyesho ya kuchukiza ya rais huyo , na baadaye mwanamke huyo alikaririwa akisema kuwa "hakuna uovu" katika busu.Hii si mara ya kwanza kwa raisi Duterte kushutumiwa kutokana na tabia zake mbaya dhidi ya wanawake.

Kama hiyo haitoshi wanawake wawili wa Ufilipino walialikwa kupanda jukwaani ili kupokea nakala ya bure ya kitabu, na walikuwa na bashasha tele na nyota zao kung'aa kutokana na kitencho cha kusimama karibu na raisi Duterte.

Mwanamke huyo baadaye alifahamika kwa jina la Bea Kim, na kunukuliwa na vyombo vya habari vya Ufilipino akijinasibu ya kuwa baadaye raisi alimuuliza kama ameolewa ama lah, ingawa alimuarifu kuwa ameolewa na raia wa Korea.Pia amekiteteta kitendo cha raisi na kusema kuwa hakukuwa na nia yoyote mbaya, na kuongeza kuwa lengo lilikuwa kuwaburudisha wafilipino waliokusanyika.Wafuatiliaji wa mambo wanaarifu kuwa raisi anayafanya yote haya ili kufunika mfululizo wa mauaji nchini mwake , ili machoni pa mataifa aonekane mwema.

Mnamo mwaka 2016, alizungumza kwenye mkutano wa kampeni za kugombea nafasi ya uraisi kuhusiana na kesi ya ubakaji na mauaji iliyotukia mwaka 1989 iliyomhusu mfanyakazi wa kimishionari aliyekuwa katika mji wa Davao, ambapo yeye alikuwa meya wa mji huo , kwamba alichukizwa na kitendo cha kubakwa mwanamke huyo, hilo ni jambo moja, lakini alikuwa ni mwanamke mzuuuuri, kwahakika meya angepaswa kuwa mtu wa kwanza kukutana kimwili na mwanamke huyo, hasara gani hiyo iliyosababishwa, ingawa baadaye ofisi yake iliomba radhi kutokana na matamshi hayo.

Maoema mwaka huu, Raisi Durtete aliwapa maelekezo askari wake kuwa wanapaswa kuwapiga risasi sehemu za siri wanawake waasi wenye misimamo ya kijamaa, matukio hayo yote hayo mawili yalisababisha upinzani mkali kwenye mitandao ya kijamii.

Howard Johnson, mwandishi wa BBC aliyeko nchini Phillipins anaarifu kuwa pamoja na upinzani anaokabiliana nao raisi huyo, bado amesalia kuwa maarufu mara mbili nchini mwake na nje ya nchi yako ambako wapo wafanyakazi wa ki Phillipino.

Shirikisho hilo la wafanyakazi limekiri kumpenda raisi wao kwasababu ya misimamo yake ambayo inajenga taswira yenye nguvu, ya kudumu ya Philippines, na kumwita kuwa ni baba wa takwimu mwenye kufuatilia watoto wake wanafanyao kazi nje ya nchi.

Mwandishi Howard anasema kuwa alikuwa nchini Uingereza na kufanikiwa kukutana na nesi mmoja mwenye asili ya Ufilipino anayefanya kazi mjini London. Yeyey anaona kuwa vyombo vya habari vya kimagharibi vina vyombo vya habari vya Magharibi vinaandika habari zimhusuzo raisi huyo bila mizania na wanaandika bila ya weledi .

Zaidi ya hayo kuna tetesi kuwa wanadayaspora wamekuwa walengwa wakuu wa mitandao ya twitter na Facebook na lengo ni kuharibu hadhi ya raisi.