Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Waajiri wanatafuta mchanganyiko wa ujuzi kama vile ubunifu,ushawishi na ushirikiano kazini
Kila mwaka watu hujiwekea maazimio mapya kwa lengo la kujiimarisha katika nyanja tofauti maishani.
Wengine wanapotafuta kazi wale walio na kazi wanatafakari ni jinsi gani wanaweza kujiendeleza katika taaluma zao.
Ili kutoa muongozo kwa watu wanaotafuta kazi watafiti watafiti kutoka baraza la kiuchumi duniani waliamua kulivalia njuga suala hilo.
Katika ripoti yao mpya kwa jina ''Hatima ya baadae ya kazi'',wataalamu wa baraza hilo walijaribu kuunganisha teknolojia mpya na zile zinazojitokeza ili kutathmini kiwango cha juu cha ufanisi kazini.
Lengo lao lilikua kuelewa uwezo wa teknolojia mpya katika mpango wa kuunda ajira mpya na kuboresha kazi ya makampuni ya uzalishaji.
Matokeo yaliyotokana na uchambuzi kutoka kwenye tovuti ya mtandao wa LinkedIn, yamebaini kuwa waajiri wa 2019 wanatafuta mchanganyiko wa ujuzi pamoja na ubunifu.
Baadhi ya ujuzi unaotafutwa na waajiri mwaka huu ni pamoja na "Kujiimarisha kiujuzi katika kazi husika, na kuhakikisha unakwenda na wakati," aliandika mhariri wa LinkedIn, Paul Petrone katika blogu moja.
Mchanganyiko wa ujuzi
Pamoja na kukua kwa sekta ya viwanda,waajiri wanatafuta mchanganyiko mkubwa wa ujuzi.
Huku teknolojia ikiendelea kuimarika inatoa nafasi mpya za kazi zinazohitaji ujuzi wa hali ya juu.
Hali hiyo inaleta ushindani unaofanya kazi zingine kupitwa na wakati
Ujuzi wa hali ya juu pia umekuja na mahitaji ya mbinu madhubuti ya kuhifadhi data kutokana na kuimarika kwa teknolijia ya dijitali duniani.
Mbali na ubunifu, LinkedIn imesema kuwa ujuzi mwingine kama vile ushawishi, ushirikiano, uwezo wa kumudu mazingira tofuti ya kazi na kuzingatia muda wa kazi ni muhimu.
Watafiti walichunguza iwapo kuna uwezekano wa vigezo hivyo kubadilika siku zijazo wakizingatia vigezo hivyo.
Kazi tano zinazolengwa na waajiri mwaka 2019
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtandao wa LinkedIn unawaleta pamoja waajiri na waajiriwa hizi ndizo kazi zinazolengwa na waajiri mwaka 2019
- Ubunifu
- Ushawishi
- ushirikiano
- kumudu mazingira tofuti ya kazi
- Usimamizi wa muda
Ujio wa roboti
Kwa mujibu wa utafiti suala la kuimarika kwa ujuzi bado linayumba yumba kutokana na teknolojia kubadilika mara kwa mara.
Hii inaamaanisha teknolojia ikibadilika ujuzi mpya unahitajika kufanya kazi husika.
Inakadiriwa kuwa nusu ya wafanyikazi watalazimika kutafuta upya ujuzi la sivyo watapoteza nafasi zao za kazi miaka michache ijayo.
Watunzi wa sera sasa hawana budi kubuni mbinu mbadala ya kukabiliana na mabadiliko yanayoshuhudiwa katika sekta ya ajira.
"Mabadiliko yanayoshuhudiwa katika sekta ya ajira kwa sasa yatatitumia wafanyakazi wengine huku ikibuni fursa mpya za kazi kwa wengine," ilisema ripoti hiyo.
Moja ya changamoto wanazukutana nazo watu wanaotafuta kazi ni kutokufahamu waajiri wanataka nini.
Hali hiyo huwafanya kutoa taarifa zisizo sahihi au zisizohitajika kwenye usaili.
Kujua nini waajiriwa wanatafuta kwenye usaili humsaidia msailiwa kuandaa taarifa zilizo sahihi kumuwezesha kushida katika usaili.
Unapoitwa kwenye usaili inamaanisha kuwa umeshafikia vigezo vya kupewa kazi kwa kuzingatia taarifa za awali alizotoa kupitia wasifu na barua ya kuomba kazi.
Waajiri wanatafuta sifa zipi?
- Kujiamini-Hili ni suala la muhimu sana katika utendaji wa kazi. Wasailiwa wengi huonesha uoga na wasiwasi hata kabla hawajaanza kujibu maswali.
- Ubunifu-Taasisi nyingi zinakumbana na changamoto ya ushindani hivyo waajiri hupenda kuajiri watu wenye sifa ya ubunifu.
- Ujuzi na uwezo wa kufanya kazi husika-Ufaulu unaonekana kwenye vyeti hautoshi kuthibitisha kuwa msailiwa anafaa kwenye nafasi aliyoiomba. Ujuzi na uwezo wa kazi hutathminiwa kupitia uzoefu alionao msailiwa.
- Taarifa kuhusu nafasi unayotarajia kupewa-Ni muhimu kufanya utafiti juu ya taasisi kabla ya kwenda kwenye usajili. Mara nyingi taarifa hizi hupatikana kwenye tovuti ya taasisi husika na kupitia watu wanaofanya kazi na taasisi hiyo.
- Ujuzi katika mawasilino- Kubaini kama una uwezo mzuri katika kuwasiliana wasaili huangalia matumizi ya lugha katika kujibu maswali; hii hujumuisha matumizi sahihi ya maneno, matamshi na lugha ya mwili kama kutumia mikono na muonekano wa sura.
Vigezo vingine ni pamoja na
- Matarajio yenye uhalisia-Ni dhahiri kuwa hakuna muajiri atakaye kuajiri kama hana uwezo kufikia matarajio yako. Hii inajumuisha matarajio ya kiwango cha mshahara; kama utataja mshahara mkubwa ambao taasisi itashindwa kukulipa inaweza ikawa sababu ya kukosa ajira.
- Uwezo wa kumudu mazingira tofauti tofuti ya kazi-Ufanisi na tija kazini hutegemea uwezo wa mfanyakazi kuweza kumudu mazingira tofauti tofauti ya kazi.
- Kitu cha ziada utakacho ongeza kwenye taasisi-Mara nyingi waajiri hawapendi kumpa kazi mtu wa kawaida. Kando na uwezo wako wa kufanya kazi ni nini cha ziada utakacho kiongeza kwenye taasisi au kazi husika.
- Utayari wa kujifunza-Ni vyema katika maelezo yako kuonesha kuwa unapenda kujifunza na uko tayari kuongeza ujuzi wako pale fursa itakapopatikana.
- Uwezo wa kujitambua-Uwezo wa kijifanyia tathimini na kujua sifa ulizonazo ikiwemo udhaifu ulionao unaweza husaidia kutoa taarifa zitakazoonesha kuwa unajitambua.