Kwa miaka 40 fuvu la Mangi Meli kutoka Tanzania limekuwa likitafutwa nchini Ujerumani

Chanzo cha picha, Tahir Della
Shinikizo linazidi kuongezeka nchini Ujerumani na Uingereza kuzitaka nchi hizo kurejesha mafuvu yaliyotolewa Afrika kwa utafiti zaidi ya karne moja iliyopita.
Raia wa Tanzania anayeishi nchini Ujerumani Mnyaka Sururu Mboro, amekuwa akitafuta fuvu lililotoweka la Mangi Meli kwa miaka 40.
Mangi Meli, chifu kutoka eneo la kaskazini ya sasa ya Tanzania aliuawa mwaka 1900 kwa kupambana dhidi ya utawala wa ukoloni wa Ujerumani.
Baada ya kuuawa mwili wake uliakatwakatwa na kichwa chake kikasafirishwa kwenda nchini Ujerumani.
Lilipo fuvu lake bado haijulikani, lakini baada ya wakfu unaofahamika kama Prussian Cultural Heritage wa mjini Berlin kugundua mafuvu zaidi kutoka Tanzania, imempa Bw Mboro matumaini mengi.

Chanzo cha picha, National Museums in Berlin
Anatoka eneo sawa na alilokuwa akitoka Mangi Meli, na mwaka 1977, kabla hajaondoka kwenda kusoma Ujerumani alimuambia bibi yake kuwa angetafua fuvu hilo.
Watafiti wamegundua mabaki 200 kutoka Tanzania mengi yakiwa ni mafuvu ambayo yalichukuliwa wakati nchi bado ilikuwa chini ya utawala wa Ujerumani.
Tangu Oktoba mwaka 2017 wamekuwa wakichunguza ilikotoka mifupa iliyo kwenye hifadhi yao ambayo inatajwa sasa kuwa maelfu.
Mradi wao ulianza mwaka mmoja baada ya mwandishi wa habari raia wa Ujerumani kufichua kiwango cha mabaki kutoka nchi zilizokuwa makoloni ya Ujerumani.
Watafiti pia wametambua mafuvu 900 kutoka Rwanda na takriban kati ya 400-500 kutoka Togo na Cameroon - hizi ni nchi zilizokuwa sehemu ya makoloni ya Ujerumani kati ya mwaka 1884 na 1918.

Chanzo cha picha, National Museums in Berlin
Maziko mazuri yatakiwa
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga amesema serikali inataka kujadili kurejeshwa mabaki hayo.
Maziko mazuri ndicho kilicho akilini mwa Bw Mboro.
Anasema kuwa ikiwa atarejesha fuvu la Mangi Meli kwenda Moshi kaskania mwa Tanzania atapata amani kwa kuwa mwili chifu huyo uliokatwa unahitaji kukamilika.
Bw Mboro ambaye sasa anaishia mjini Berlin anatoka jamii sawa na ile ya Chifu Meeli aliyeuawa na alikuwa akiambiwa hadithi za ujasiri wake.
Nyanya yake alimwambia jinsi alibaki muasi hadi siku ya kifo chake.
Mangi Meli alinyongwa pamoja na watu wengine 18 lakini alichukua muda wa saa saba kufa ishara ya jinsi alikuwa jasiri, Bw Mboro alisema.

Chanzo cha picha, AFP
Bw Mboro alikuwa ametumia miongo minne kushinikiza mamlaka kufungua makavazi na kuangalia mabaki hayo ya binadamu.
Kwanza ilikuwa ni kupuuza kuliko kakataa ndiyo ilizuia kutafutwa, anasema.
"Kila mtu niliyekuwa nikimuuliza alisema hakufahamu chote kuhusu historia."
Lakini baadaye aligundua kuwa makavazi ya Charité mjini Berlin yalikuwa na mafuvu na mwaka na 2000 wataalamu wawili waliruhusiwa kuyatazama.
Waligundua kuwa kulikuwa na takriban mafuvu 70 kutoka Tanzania, lakini kulingana na rekodi hakukuwa na vuvu la Mangi Meli.

Kwa Bw Mboro matumaini ni kuwa vuvu la Mangi Meli litarejeshwa, anaendea kusubiri licha ya serikali yake kuonyesha nia ya kurudisha mabaki ya watu.
Lakini Bw Mboro anahisi ni hali nyingine kuchelewa tena na anahofu huenda asitimize ahadi alitoa kwa bibi yake.












