Mafuvu ya kale yatafutiwa kwao

Mafuvu

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Watafiti hao wataweka bayana utafiti wao hivi karibuni

Nchi ya Ujerumani imeanza kufanya uchunguzi ili kugundua asili ya mafuvu zaidi ya elfu moja kutoka katika koloni lake la zamani Afrika Mashariki.

Yaliyo mengi yanaaminika kutoka katika nchi ya Rwanda. Inaaminika kuwa mafuvu hayo yalisafirishwa kwa njia ya meli na kuingizwa nchini Ujerumani miaka mia moja iliyopita kwa shughuli za kujifunza hasa kwa mwanadamu anayejifunza maendeleo ya wanadamu.

Wahifadhi wa mali kale nchini Ujerumani walitumia miongo kadhaa katika kuyahifadhi na kwa sasa mafuvu hayo yameharibika sana.

Mafuvu hayo sasa yameunganishwa tena lakini nyaraka nyingi kuhusiana nayo nyingi zimekwisha potea.

Watafiti wanasema dalili bora zaidi ni maelezo yaliyoandikwa kwenye mifupa yenyewe kwa sasa.