Mauaji ya kimbari: Ujerumani yarejesha mafuvu ya watu iliowaua Namibia 1904

Herero woman in traditional dress

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mwanaharakati wa Herero Esther Muinjangue bado anataka msamaha kutoka serikali ya Ujerumani

Ujerumani imerejesha mabaki ya binadamu ya watu wa asilia waliouawa wakati wa mauaji ya kimbari wakati wa ukoloni zaidi ya miaka 100 iliyopita.

Ujumbe wa serikali ya Namibia ulipokea mafuvu hayo wakati wa ibada ya kanisa kwenye mji mkuu Berlin.

Mifupa hiyo ilikuwa imetimwa kwenda Ujerumani kufanyiwa utafiti kubaini uwezo wa wazungu.

Maelfu ya watu wa Horero na Nama waliuawa walipokuwa wakipinga ukoloni.

Vizazi vyao bado vinasubiri msamaha kutoka kwa serikali ya Ujerumani.

Kwa nini mauaji hayo yakatokea?

Mauaji hayo yalianza mwaka 1904 baada ya jamii za Herero na Nama kuasi baada ya wajerumani kuchukua mashamba yao na mifugo.

Mkuu wa jeshi wa ile iliyojulikana kama German South West Africa, Lothar von Trotha alitoa amri ya kuuliwa watu Oktoba mwaka 1904.

Herero na Nama walisukumwa kwenda jangwani na yeyote ambaye alipatikana akirudi kwenda kwa ardhi yao aliuawa au kupelekwa kwenye zenye misongamano.

Troops in German South West Africa (now Namibia) at the time of the Herero revolt of 1904

Chanzo cha picha, Hulton Archive

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Ujerumani waliuaa wakabaka na kuwafanya watu watumwa

Hakuna idadi kamili ya watu waliouawa na makadirio mengine yamewekwa kuwa takriban watu 100,000.

Inaaminiwa kuwa asilimia 75 ya watu wa Horero na nusu ya watu wa Nama walikufa.

Mafuvu ya baadhi ya wale walio uawa yalitumwa kwenda nchini Ujerumani ambapo wasayansi waliyafanyia uchunguzi kama njia ya kubaini ukweli kuhusu uwezo wa wazungu.

A skull with a catalogue number on it

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mafuvu yalikuwa sehemu ya mabaki ya binadamu yaliyofanyiwa utafiti nchini Ujerumani

Inaamiwa kuwa kuna mamia ya mafuvu ya raia wa Namibia nchini Ujerumani na leo Jumatano zaidi ya mafuvu 25 yalisalimishwa.

Mafuvu kutoka koloni zingine za Ujerumani zikiwemo Cameroon, Tanzania, Rwanda na Togo yalitumwa kwa utafiti huo.

Ujerumani itaomba msamaha?

Mwaka 2016 Ujerumani ilisema ilikuwa inajiandaaa kuomba msamaha lakini bado inajalidiliana na serikali ya Namibia njia ya kuomba msamaha huo.

Sherehe ya leo Jumatano ndiyo mara ya tatu ambapo mabaki yanarejeshwa Namibia lakini kulikuwa na matumaini kuwa mara hii kungekuwa na mapatano kamili.

Vizazi vya waathiriwa vina machungua kuwa hukujakuwepo msamaha na makubaliano ya fidia. Pia wana hasira kuwa hawajashirikishwa kweney mapatano hayo.

Church service

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mabaki hayo sasa yatapelekwa nchini Namibia