Vitisho vya mabomu Marekani: Tunafahamu nini kuhusu vifurushi vinavyotiliwa shaka kuwa ni vilipuzi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Vifurushi kadhaa vinavyodhaniwa kuwa ni vifaa vya vilipuzi ambavyo rais Donald Trump alivikosoa vinaendelea kuchunguzwa na mamlaka nchini Marekani.
Kutoka New York mpaka Los Angeles na kutoka Washington mpaka Florida, vifaa hivyo viliripotiwa kuwa ni jambo ambalo sio la kawaida na vilitumwa katika bahasha ambazo zinafanana.
Hakuna kifurushi hata kimoja ambacho kililipuka na shirika la kijasusi wameanza kufanya uchunguzi.
Shirika hilo la kijasusi limeanza msako eneo la Miami, wakati ambao wachunguzi wanajaribu kuona ni nani anahusika na vilipuzi hivyo.
Vifaa hivyo vimetumwa kwa watu 8 mashuhuri akiwemo rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na muigizaji Robert De Niro.
Maafisa ambao hawakujitambulish majina yao waliviambia vyombo vya habari vya Marekani kuwa wachunguzi wanaamini kuwa inaaminika kuwa kifurushi kimoja kilitumwa kutoka Florida.
Vifurushi vya aina hiyohiyo vilitumwa kwa makamu wa rais wa zamani Joe Biden na katibu wa taifa hilo Hillary Clinton,
Shirika la kijasusi FBI haijatoa ripoti yeyote kuhusu uchunguzi wanaoufanya.
Na haya ndio tunayafahamu.
Walengwa ni akina nani?
Kifaa cha kwanza kuonekana katika sanduku la barua karibu na nyumba ya bilionea mfanyabiashara Soros huko New york mwezi Oktoba tarehe 22.
Bwana Soro ,mfadhili wa chama cha Democratic , amekuwa mara kwa mara akikosolewa kwa kuwa upande wa upinzani.
Kifaa hicho kiligunduliwa na mfanyakazi mmoja na baadae kifaa hicho kiliharibiwa na maafisa.
Polisi wanasema kuwa vifurushi hivyo vilikuwa vinajumuisha unga wa poda inayolipuka na imetengenezwa na vitu vinavyotengenezwa na bomu.

Chanzo cha picha, Empics
Siku iliyofuata idara ya huduma za siri iligundua kuwa kifurushi kilichotumwa kwa bi.Hillary Clinton ambaye alikuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Democratic na katibu wa zamani wa Marekani.
Imeripotiwa kuwa uchunguzi wa barua hizo zilizotumwa alimshirikisha mume wake ambaye ni rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton huko Chappaqua, New York.
Afisa wa Marekani aliwaambia waandishi wa habari kuwa kilikuwa ni kifaa kinachoweza kulipuka.
Kifurushi cha tatu ambacho kilitumwa kwa rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, kilitumwa tarehe 24 mwezi oktoba mjini Washington Dc.
Vifurushi hivi vilikuwa vinapelekwa katika maeneo ambayo yalilengwa, tamko lililotolewa na idara ya huduma ya siri ilielezea matukio yote mawili.
Waandamaji hawakupata vifurushi hivyo wala kupata vitisho vya kupokea vifurushi vipi, idara hiyo iliongeza.

Tukio lingine lilitokea katika ofisi za CNN mjini New York ziligunduliwa siku ya jumatano asubuhi baada ya kudhania kuwa kuna bomu lilitumwa katika chumba chao barua.
Ilielezwa kuwa mkurugenzi wa zamani wa CIA John Brennan,ambaye huwa anamkosoa rais Trump, alikuwa amepangwa kuonekana katika kipindi cha The network.
Polisi wanasema kuwa walikuta bahasha iliyokuwa na unga mweupe wa poda katika kifaa hicho ambacho pia kinafanyiwa uchunguzi.
Kipindi kilikuwa hewani wakati kifurushi hicho kilipobainika na kengele ya tahadhari iliposikika, wakati watangazaji wakijadili stori.
Baadae siku hiyohiyo, ripoti ziloonyesha kuwa wakili mkuu wa zamani Eric Holder alikuwa ametumiwa kifaa kinacholipuka.
Na taarifa nyingine kuwa kuna kifaa kingine kilitumwa kwa Maxine Waters ambaye ni mshirika wa Democratic kimeonekana katika eneo la kupokea barua karibu na mji wa Washington, DC.
Kifurushi kingine ambacho kilishukiwa na kiliandikwa jina lake kilionekana Los Angeles.

Chanzo cha picha, Getty Images
Siku ya alhamisi, Kifurushi kingine kilitumwa katika mgahawa ambao unamilikiwa na muigizaji Robert De Niro.
Baadae FBI walidhibitisha kuwa kuna vifaa vingine ambavyo vilitiliwa shaka vilivyotumwa kwa makamu wa raisi wa zamani Joe Biden huko Delaware.
Tunafahamu nini kuhusu vifurushi hivyo?
Hakuna kifurushi hata kimoja ambacho kililipuka au kusababisha madhara yeyote mpaka sasa.
Vifurushi vyote vilikuwa vimefungwa katika bahasha ya manila, zikiwa zimeandikwa kwa maandishi ya kompyuta na mtumaji akiwa ameandikwa Debbie Wasserman Schultz, ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya chama cha Democratic ingawa jina hilo lilikuwa halijaandikwa kiusahihi.
Mwanamke huyo mwanasiasa kutoka Florida ameeleza masikitiko yake kwa jina lake kutumika.
Kifaa hicho kilisadikiwa kuwa ni bomu . Kifaa kilichotumwa katika ofisi za CNN ambazo picha yake inaonyesha kifaa hicho kilizungushiwa gundi ya karatasi ya rangi nyeusi.
Wakala wa Shirika la kijasusi la FBI Bryan Paarman aliwaambia waandishi wa habari kuwa kifaa hiki kilikuwa kinafanya kazi.
Maafisa hawakusema kama vifurushi hivyo vilikuwa ni bomu na wachunguzi wanafanyia kazi kuhakikisha hilo
Uchunguzi uliofanyika unaonyesha kuwa vifaa hivyo vinavyosadikiwa kuwa ni vilipuzi vilikuwa vinafanana.

Chanzo cha picha, CNN/AFP
Hatua gani zimechukuliwa?
Matukio hayo yameshukiwa kuwa ni ya kisiasa.
Chama cha Conservatives kudai kuwa Democrats wamelenga kuhamasisha chuki kwa kuweka vitisho vya bomu.
Rais Trump ameviambia vyombo vya habari kuacha kutoa taarifa zinazohamasisha chuki baada ya tukio hilo kutokea.
Lakini kauli yake ilikosolewa na kudaiwa kuwa huwa anatumia lugha ambazo sio nzuri kwa wapinzani na waandishi wa habari.
Raisi wa shirika la habari la kimataifa CCN Jeff Zucker alidai White house imekosa kuwa waelewa kabisa na haizingatii suala ya mashambulizi katika vyombo vya habari.















