Sakata la vilipuzi:Donald Trump avishambulia vyombo vya habari

Rais Donald Trump amevitaka vyombo vya habari kusitisha chuki isiyokuwa na kikomo baada ya kutoa taarifa ya kudhania kuwa vilipuzi vilikuwa vimetumwa kwa watu mashuhuri nchini Marekani.
Alizungumza hayo baada ya vifurushi hivyo kutumwa kwenye chombo cha habari cha CNN na viongozi wa juu wa chama cha Democrats ikiwajumuisha Barack Obama na Hillary Clinton.
Mpaka sasa hakuna kifurushi chochote kilicholipuka.
Shirika la ujasusi la FBI linawatafuta waliotuma mizigo hiyo.
Rais kukosoa jambo hilo linaonyesha ishara ya kutokuwa mkweli kwa sababu ni kawaida yake kutumia lugha zisizokuwa rafiki kwa vyombo vya habari na wapinzani wake.
Rais Trump alizungumza jana na kudai kuwa atahakikisha watu waliotuma vifurushi hivyo watakamatwa huku akiwataka vyombo vya habari kuacha kutoa taarifa ambazo hazina ukweli wowote.
Trump aliwataka watu kuwa watulivu na kusema matukio kama haya yanayohusisha masuala ya kisiasa yanapaswa kuisha na yasisababishe wanasiasa kutoelewana.
Mtu yeyote hapaswi kufananisha upinzani wa kisiasa na mashujaa wa kihistoria, jambo ambalo linafanyika mara kwa mara.
Hata hivyo rais Trump hakuweka wazi ni jambo gani ambalo amelenga kuwafanyia waliotuma mizigo hiyo.
Mapema Mkurugenzi wa shirika la habari la CNN Jeff Zucker alimkosoa rais Trump na katibu wa habari wa Ikulu ya white house kwa kutoelewa kuwa maneno yao yanaweza kuleta athari.
Hii inaonyesha wazi kabisa kuwa anakosa uelewa juu ya ubaya wa ongezeko la mashambulizi ya vyombo vya habari .
Ni watu gani walitumiwa vifurushi hivyo?

Chanzo cha picha, Getty Images
Vifurushi vilivyodhaniwa kuwa ni vilipuzi vilitumwa mjini New York, Washington DC na Florida, mamlaka ilibainisha jana.
Vilipuzi hivyo vilitumwa kwa watu wafuatao,kwa mujibu wa shirika la kijasusi la FBI;
Katibu mkuu wa zamani,Hillary Clinton
Rais wa zamani Barack Obama
Ofisi ya mkurugenzi wa shirika la habari CNN,John Brennan
Wakili wa zamani Eric Holder
Mwanasiasa wa California kutoka chama cha Democratics Maxine Waters
Mfadhili na mshauri wa masuala ya fedha George Soros alitumiwa jumatatu
Ofisi za shirika la habari la CNN lilifanyiwa uchunguzi jana asubuhi baada ya kupokea kifurushi kilichotumwa kwa Brennan.

Chanzo cha picha, CBS
Kifurushi kingine kinaaminika kuwa kilitumwa kwa makamu wa rais wa zamani Joe Biden na kilitakiwa na wachunguzi.
Kwa nini jambo hili limechukuliwa kisiasa?
Cha kushangaza ni kuwa watu ambao wamelengwa ni wa upande wa Democratic na chama cha conservatives wamekuwa wakikosoa jambo hilo haswa rais Trump.
Baadhi ya wanachama wa Democrats wamemshutumu rais kuhusika na uhalifu huo huku baadhi ya wafuasi wake wanaamini kwamba vifurushi hivyo vinavyodhaniwa kuwa ni vilipuzi viliwekwa na Democratic wenyewe ili waweze kupata kura wakati wa uchaguzi .
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Hakuna ushaidi wowote kuhusu jambo hili na polisi hawajatoa tamko lolote kuhusu kushukiwa kwa yeyote.
Majaribio hayo ya mashambulizi yamekuja ndani ya wiki mbili kabla ya uchaguzi mdogo ambapo wanasiasa wa Marekani wakiwa na mgawanyiko.
Hatua gani zimechukuliwa?

Chanzo cha picha, Getty Images
Awali meya wa New York Bill de Blasio amesema jaribio la mashambulizi yaliyotokea katika ofisi za shirika la habari CNN na viongozi wa juu wa chama cha Democrats uikiwajumuisha Barack Obama na Hillary Clinton,ni jaribio la kigaidi.
Bwana de Blasio aliwaambia waandishi wa habari kuwa ni rais kuwea ijtihada za kuwatisha na kukandamiza uhuru wa habari na viongozi wan chi hii kwa njia ya uhalifu.
Jana msemaji wa White house,bi Sarah Sanders alilaani majaribio hayo ya uhalifu dhidi ya watu mashuhuri na.Vilevile aliweka msisitizo katika ujumbe wake wa twitter kuwa White House inalaani vikali vitisho vilivyotolewa dhidi ya shirika la habari la CNN.

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais alirudia na kuwaita waandishi wa habari na haswa CNN kuwa habari za uongo na kuongeza chuki kwa watu.
Wiki iliyopita alimsifu mwanasiasa wa Republican ameye alimtusi mwandishi wa habari.
Kwa pamoja viongozi wa Democrats Nancy Pelosi na Chuck Schumer walisema pia maneno hayo ya rais ni mazito na anapaswa kukemea vitendo vya uhalifu.
Katika mkutano na waandishi wa habari Meya de Blasio aliongeza kuwa maafisa wote na watu wote kwa ujumla msisitize uhalifu,msisitize chuki wala mashambulizi katika vyombo vya habari na vyema uonyesha heshima.
Shirika la kijasusi la FBI linasema kipaumbele chake kwa sasa ni kufanya uchunguzi jambo hilo.
Kitu gani kilikuwepo katika kifurushi?
vifaa ambavyo vinasadikiwa kuwa ni mabomu ingawa hakuna hata kimoja kilicholipuka.
Vifurushi vilivyotumwa kwa Obama na Clinton vilikamatwa na walinzi kabla havijawafikia.
Vifurushi hivi ambavyo vyote vilikuwa vimefungwa na karatasi ya manila, zikiwa zimeandikwa na maandishi ya komputa .

Chanzo cha picha, FBI
Katika kila barua jina lililoandikwa kuwa zimetoka kwa Debbie Wasserman Schultz, mwanasiasa wa zamani wa Democratic .
Katika maelezo yake,mwanasiasa huyo wa zamani wa Florida amesema kuwa
jambo hili limewachanganya sana na haswa jina lake lilipotumika.












