Kifaa kinachodhaniwa kuwa kinalipuka kimetumwa nyumbani kwa Clinton na Obama

Chanzo cha picha, Getty Images
Kifaa kinachosadikiwa kuwa ni mlipuko kimebainika katika nyumba ya Bill na na Hillary Clinton leo hii, maafisa wa sheria wameiviambia vyombo vya habari nchini Marekani.
Aina ya kifurushi kinachoshukiwa kimetaarifiwa kutumwa pia katika ofisi za rais wa zamani wa Marekani Barack Obama.
Ni siku mbili baada ya bomu kurushwa katika nyumba ya mfadhili na mshauri wa mambo ya fedha George Soros huko mjini New York.
Clinton ambaye ni rais wa zamani wa Marekani na mke wake Bi.Clinton ambaye aliwania urais mwaka 2016.
Taarifa zilizoripotiwa na New York Times zimesema kwamba kitu hicho kilibainika kuwa kinalipuka baada ya fundi kukifanyia uchunguzi.
Kifaa hicho kiliacha kilomita 65 kaskazini mwa mji wa New York.

Chanzo cha picha, Getty Images
Haijawekwa wazi kuwa kifaa hicho kinachotiliwa shaka kilionekana wapi.
Hata hivyo msemaji wa Obama amekana kuwepo kwa tukio hilo na kuwataka waandishi kushirikiana na idara ya huduma ya maelezo ya siri.
Maafisa wakuu wa White House wameiambia NBC kwamba rais Donald Trump tayari ameshapata taarifa kuhusu jambo hilo.
Msemaji wa Ikulu Sarah Sanders amelaani jaribio hilo la mashambulio ya vurugu dhidi ya watu mashuhuri.
"Matukio ya kigaidi hayakubaliki popote na mtu yeyote ambaye atakamatwa kuhusika atachukuliwa sheria
Uchunguzi bado unaendelea ili hatua sahihi ziweze kuchukuliwa" Msemaji wa Whitehouse Sarah Sanders .
Kifaa cha aina hiyo kiliwahi kutumwa katika ofisi za CNN mjini New York ambapo iliwalazimu waandishi wa habari kukatisha matangazo mara baada ya kusikia kengele ya moto.












